Watu wa eneo la Catalonia nchini Uhispania wameanza kupiga kura katika uchaguzi uunaotazamwa kuwa mtihani mkubwa wa kuunga mkono Uhuru wa eneo hilo tajiri.
Zaidi ya watu milioni tano wamejiandikisha kupiga kura .
Wanachama wa vyama vya Catalan, wanaotaka kujitenga na ambao wanaongoza katika kura ya maoni wanasema kuwa ushindi utavipa vyama vyao uwezo wa kutangaza
kwa kauli moja uhuru wao.
Serikali ya Uhispania ambayo inakataa kata kata kukubalia shughuli hizo za upigaji wa kura ya maoni kuhusiana na swala hilo imetaja kura hiyo ya maoni kama upuzi
mtupu.
Uchaguzi huo unaonekana kama swala muhimu katika historia ya hivi punde ya Uhispania.
No comments:
Post a Comment