TANGAZO


Wednesday, August 12, 2015

Watu wa China wazindua Kampeni ya kuwalinda wanyama dhidi ya Ujangili

Balozi wa China nchini Tanzania, Dk. Lu Youqing (katikati), akihutubia wakati akizindua kampeni ya kupambana na ujangili viwanja vya Leaders Club Dar es Salaam leo asubuhi. Kampeni hiyo imeanzishwa na watu wa China kwa ajili ya kuunga jitihada za watanzania katika mapambano hayo ya kuwalinda wanyama dhidi ya ujangili hasa tembo.
Balozi wa China nchini Tanzania, Dk.Lu Youqing (kulia), akimpa zawadi ya mpira kwa niaba ya wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Kinondoni, Faudhia Eddy katika uzinduzi huo. Balozi huyo alitoa zawadi ya mipira kwa baadhi ya shule za Manispaa ya Kinondoni.
Balozi wa China nchini Tanzania, Dk. Lu Youqing (kulia), akimpa zawadi ya mpira, Mwalimu Flora Lukali kutoka Shule ya Mount Pleasant kwa ajili ya shule hiyo.
Balozi wa China nchini Tanzania, Dk. Lu Youqing akionyesha umahiri wa kuchezea mpira katika uzinduzi huo kabla ya kutoa zawadi ya mipira kwa baadhi ya shule za Manispaa ya Kinondoni.
Wanafunzi wakiwa na vipeperushi vya bendera ya nchi ya china wakati wa uzinduzi huo.
Wasanii wa kundi la makhirikhiri wakitoa burudani katika uzinduzi huo.
Wanafunzi wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Wimbo wa Taifa ukiimbwa.
Wanahabari wakichukua taarifa za uzinduzi huo.
Wanafunzi ndani ya uzinduzi huo. (Imeandaliwa Dotto Mwaibale) 

No comments:

Post a Comment