TANGAZO


Wednesday, August 12, 2015

Vodacom na TFF zasaini mkataba wa udhamini wa ligi kuu kwa miaka mitatu

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Jamali Malinzi(kulia)akiongea na waandishi wa habari wakati wa hafla fupi ya kusaini mkataba mpya wa miaka (3) wa kudhamini ligi Kuu ya  Vodacom Tanzania  bara kwa msimu wa 2015/16. Katikati ni Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa kampuni hiyo Kelvin Twissa na kushoto ni Ofisa Mkuu mtendaji wa ligi Boniface Wambura. (Picha zote na Mpigapicha wetu)
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamali Malinzi(kushoto)na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa kampuni hiyo Kelvin Twissa (kulia) wakielekezwa na Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu jinsi ya kusaini mkataba wa makubaliano ya udhamini wa ligi Kuu ya  Vodacom Tanzania  bara kwa msimu wa 2015/16. 
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamali Malinzi (kushoto) pamoja na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa kampuni hiyo Kelvin Twissa (katikati)wakisaini mkataba mpya wa miaka(3) kwa Vodacom Tanzania kuendelea kuwa mdhamini mkuu wa ligi Kuu ya  Vodacom Tanzania  bara 2015/16. Anayeshuhudia kulia ni Ofisa Mkuu mtendaji wa ligi Boniface Wambura. 
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kwenye hafla fupi ya kusaini mkataba mpya wa miaka (3) baina ya Vodacom Tanzania na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa Kampuni hiyo kuendelea kuwa mdhamini mkuu wa ligi Kuu ya  Vodacom Tanzania  bara 2015/16. 
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamali Malinzi(kushoto) na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa (katikati) wakibadilishana nyaraka za mkataba wa makubaliano ya kampuni hiyo kuendelea kuwa mdhamini mkuu wa ligi kuu  ya  Vodacom Tanzania  bara 2015/16 kwa miaka (3) anayeshuhudia kulia ni Ofisa Mkuu mtendaji wa ligi Boniface Wambura.
Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa (katikati) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na mkataba mpya wa miaka (3) wa udhamini wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara uliosainiwa baina ya Shirikisho la Mpira wa  Miguu Tanzania (TFF) na kampuni hiyo. Kushoto ni Rais wa TFF, Jamali Malinzi na kulia ni Mtendaji Mkuu Bodi ya ligi Boniface Wambura.

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
12 August 2015
SHIRIKISHO la mpira wa miguu Tanzania (TFF)  leo limeingia katika mkataba wa udhamini na mdhamini Mkuu wa ligi hiyo Vodacom Tanzania, wakati maandalizi ya ligi kuu yakiendelea.

Kampuni ya Vodacom Tanzania inayoongoza hapa nchini kwa huduma za mawasiliano imekuwa mdhamini wa ligi kuu kwa miaka minane iliyopita, na sasa imeingia mkataba mpya wa udhamini kwa miaka mitatu na TFF, mkataba utakao liwezesha shirikisho hilo kupokea fedha za udhamini kwa miaka mitatu.

Ligi kuu ya Vodacom 2015/16 inayotarajiwa kaunza  katika siku za karibuni itachezwa katika viwanja mbalimbali na kushirikisha timu 16, zikiwemo timu za Mwadui na Africa Sports ambazo zimepanda daraja msimu huu.

Mkuu wa Mawasiliano na Masoko wa kampuni hiyo Kelvin Twissa, amesema kuwa kampuni ya Vodacom iko katika mstari wa mbele katika kuunga mkono maendeleo na shughuli mbalimbali za kimichezo ndani ya nchi. 

“Wanamichezo wote ni mabalozi wazuri katika nchi. Ni wajibu wetu kuhakikisha kuwa tunawaunga mkono katika kutambua na kukuza vipaji vyao kadri tutakavyo weza,” alisema Twissa na kuongeza kuwa, “Kama jina linavyojulikana ligi kuu ya Vodacom, ligi  hii  ni maarufu nchini na nje ya nchi na inafuatiliwa na mamilioni ya washabiki wa soka nchini .”

Twissa amejivunia kampuni hiyo kuwa wadhamini wa ligi kuu kwa kipindi kingine, na kufafanua kuwa mpira wa miguu ndio unaongoza kitaifa na unapendwa na Watanzania wengi.

Mkataba huu umehusisha pande zote ambazo ni kampuni ya Vodacom Tanzania, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kamati ya ligi.

Kwa upande wake Rais wa TFF, Jamali Malinzi, ameipongeza kampuni ya Vodacom Tanzania akisema kuwa anaamini kuwa maendeleo ya sasa yatalenga zaidi katika kuunga mkono vipaji vipya na vilivyopo ndani ya nchi.

“Kwa niaba ya TFF, napenda kuwashukuru Vodacom Tanzania kwa kuonyesha nia na kuendelea kuunga mkono mpira wa miguu nchini. 

Nasi tunaahidi kuendelea kuthamini vipaji vya wachezaji wetu na kuhakikisha tunapata mafanikio zaidi,” alisema Malinzi.

No comments:

Post a Comment