TANGAZO


Tuesday, August 11, 2015

Watanzania waaswa kuhifadhi mazingira

Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Sazi Salula akifungua Mkutano wa wadau wa mazingira unaohusu Miradi ya majaribio nchini wa Mkakati wa Kupunguza Uharibifu wa Misitu (MKUHUMI) leo jijini Dar es Salaam.

Kiongozi wa wawezeshaji kutoka Asasi isiyo ya kiserikali ya Niras kutoka Finland inayosimamia Miradi ya majaribio nchini wa Mkakati wa Kupunguza Uharibifu wa Misitu (MKUHUMI), Merja Makela akitoa mada wakati wa mkutano wa wadau wa mazingira kuhusu namna bora ya kuhifadhi mazingira na kuboresha usimamizi wa ardhi na kuongeza mapato kutoka kwenye misitu. Mkutano huo ambao umefanyika leo jijini Dar es salaam umeandaliwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Norway.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Sazi Salula (kushoto) akifuatilia mada wakati wa mkutano wa wadau wa mazingira kuhusu namna bora ya kuhifadhi mazingira na kuboresha usimamizi wa ardhi na kuongeza mapato kutoka kwenye misitu. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Julius Ningu.
Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa wadau wa mazingira unaohusu Miradi ya majaribio wa Mkakati wa Kupunguza Uharibifu wa Misitu (MKUHUMI) nchini wakifuatilia mada wakati wa mkutano leo jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa wadau wa mazingira unaohusu Miradi ya majaribio wa Mkakati wa Kupunguza Uharibifu wa Misitu (MKUHUMI) nchini wakifuatilia mada wakati wa mkutano leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa wadau wa mazingira unaohusu Miradi ya majaribio wa Mkakati wa Kupunguza Uharibifu wa Misitu (MKUHUMI) nchini wakifuatilia mada wakati wa mkutano leo jijini Dar es Salaam.
Mhadhiri kutoka chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof. Pius Yanda akibadilishana mawazo na Mwakilishi wa Ubalozi wa Ufaransa mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa wadau wa mazingira leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Julius Ningu (aliyevaa suti nyeusi) akiongea na baadhi ya waandishi wa habari baada ya ufunguzi wa mkutano wa wadau wa mazingira leo jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Ubalozi wa Norway nchini Tanzania (wa kwanza kushoto) akiongea na baadhi ya waandishi wa habari baada ya ufunguzi wa mkutano wa wadau wa mazingira leo jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Eleuteri Mangi-MAELEZO)

Na Jenikisa Ndile-MAELEZO

WATANZANIA wameaswa kuzingatia namna bora ya kuhifadhi mazingira, upangaji wa matumizi bora ya ardhi na utekelezaji wa mipango ili kuleta tija na maendeleo endelevu nchini. 

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Sazi Salula leo jijini Dar es salaam alipokuwa akifungua Mkutano wa wadau wa mazingira unaohusu utekelezaji wa miradi ya majaribio ya Mkakati wa Kupunguza Uharibifu wa Misitu (MKUHUMI) nchini.

Bw. Sazi alisema kuwa mipango hiyo ya MKUHUMI inalengo la kuondoa umasikini kwa watanzania waishio vijijini ambao wapo karibu na hifadhi za misitu  inasimamiwa  na kutekelezwa  kwa kushirikiana na Serikari ya kijiji ili kuhakikisha mafanikio yanapatikana kwa kuzingatia utekelezaji na usimamizi wa sheria kupitia kamati za vijiji.

Majaribio ya sera ya mazingira yamefadhiliwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Norway ili kuboresha na kushughulikia masuwala ya ardhi, misitu na kupunguza gesi joto kwa kuhimiza jamii kupanda miti kwa shughuli za maendeleo endelevu nchini.

Mipango hiyo inatekelezwa katika wilaya za Sumbawanga, Lindi, Kilwa, Zanzibar, Pemba, Kigoma na Kondoa ambapo sera hiyo imewapa elimu ya kujenga utayari wa shughuli za MKUHUMA na kuwezesha ushiriki mpana wa wadau ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Kwa upande wake Kiongozi wa miradi ya majaribio ya MKUHUMI Merja Makela alisema kuwa taasisi yake imefanikiwa kutokana na kusimamia miradi hiyo ambayo imepokelewa na kutekelezwa kama ilivyopangwa katika maeneo husika nchini.

Naye Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Julius Ningu alisema kuwa kwa tathmini iliyofanyika mwaka 2013, asilimia 55 ya ardhi ya Tanzania imefunukwa na misitu ambapo juhudi zinaendelea kufanyika kwa kuwaelimisha watanzania kuendelea kuitunza misitu hiyo kwa manufaa ya sasa na baadaye.

No comments:

Post a Comment