TANGAZO


Tuesday, August 11, 2015

Kikao cha Kamati Kuu ya CCM chaendelea Dodoma

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (CC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Alhaji Adamu Kimbisa akizungumza jambo pamoja na wajumbe wenzake Nape Nnauye na Zakhia Megji kabla ya kikao chao kilichoanza jana katika ukumbi wa NEC, mjini Dodoma leo.
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (CC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Alhaji Adamu Kimbisa (katikati), Nape Nnauye (kushoto) na Zakhia Megji wakifurahia jambo kabla ya kikao chao kilichoanza jana katika ukumbi wa NEC, Dodoma.
Mjumbe wa halmashauri kuu ya Taifa Alhaji Adamu Kimbisa akifurahia  jambo pamoja na wajumbe wenzake kabla ya kikao chao kuanza jana katika ukumbi wa NEC, Dodoma.
Wajumbe wa kamati kuu (CC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Stephen Wassira na Emanuel Nchimbi wakijadiliana jambo ndani ya ukumbi wa NEC leo.
Mwenyekiti wa CCM, Dkt, Jakaya Kikwete akiimba pamoja na Katibu Mkuu wa chama hicho leo, Abdulrahman Kinana, kabla hajafungua kikao cha Kamati Kuu iliyokutana kupitia uteuzi wa uliofanyika katika kura za maoni hivi karibuni.
Mwenyekiti wa CCM, Dkt, Jakaya Kikwete akiongoza Kikao cha Kamati Kuu (CC) mjini Dodoma leo. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu wa chama hicho leo, Abdulrahman Kinana.

Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Dkt. Salim Ahmed Salim (kulia) na Amir Kificho wakifurahia jambo wakiwa katika kakao hicho leo kabla ya kuanza kwa kikao cha kupitia uteuzi wa majina ya Ubunge. 

Dkt. Salim Ahmed Salim, Amir Kificho na Shams Vuai Nahodha ambao ni wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM wakiwa katika ukumbi wa NEC leo kabla ya kuanza kwa kikao cha kupitia uteuzi wa majina ya Ubunge.
Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia chama cha mapinduzi Samia Suluhu akiteta jambo na mjumbe mwenzake wa Kamati Kuu (CC), mjini Dodoma leo.
Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia chama cha mapinduzi Samia Suluhu akiteta jambo na mjumbe mwenzake wa Kamati Kuu (CC), mjini Dodoma leo. Kulia ni mjumbe mwenzao, Sophia Simba. (Picha zote na John Banda)  

No comments:

Post a Comment