Mashabiki wa Simba, wakifuatilia mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu kati ya timu yao hiyo dhidi ya Mwadui FC ya Shinyanga, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Timu hizo zimetoka suluhu. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Ubao wa matokeo ukionesha matokeo ya mchezo huo hadi kipindi cha kwanza kinamalizika, Simba 0 na Mwadui FC 0.
Hassan Kessy wa Simba akijaribu kumtoka Julius Mrope wa Mwadui FC.
Hassan Kessy wa Simba akipiga mpira mbele ya Julius Mrope wa Mwadui FC.
Mwinyi Kazimoto wa Simba, akiupiga mpira huku akiwa amezongwa na Juma Mnyassa wa timu ya Mwadui FC ya Shinyanga.
Papaa Niang akijaribu kuwatoka Joram Ngeveke wa Mwadui FC.
Hassan Kessy wa Simba akimtoka Juma Mnyassa wa timu ya Mwadui FC ya Shinyanga.
Awadh Juma akiwatoka wachezaji wa Mwadui FC.
Joram Ngeveke wa Mwadui FC, akiruka juu kuupiga kichwa mpira.
Mwinyi Kazimoto wa Simba, akiumiliki mpira huku akiwa amezongwa na mchezaji wa timu ya Mwadui FC ya Shinyanga.
Mwinyi Kazimoto wa Simba, akiupiga mpira huku akiwa amezongwa na Juma Mnyassa wa timu ya Mwadui FC ya Shinyanga, wakati wa mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu baina ya timu hizo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Timu hizo zimetoka suluhu.
Shaaban Kado wa Mwadui akiruka juu kuondoa mpira golini mwake.
Simon Sserunkuma akimtoka mchezaji wa Mwadui FC.
Shaaban Kado akiudakampira huku akizongwa na Mussa Hassan Mgosi wa Simba.
No comments:
Post a Comment