TANGAZO


Sunday, August 9, 2015

Nagasaki yakumbuka bomu iliyoua watu elfu 70

Nagasaki yakumbuka bomu iliyoua watu elfu 70 miaka 70 iliyopita
Ibada maalumu za ukumbusho zinaendelea kufanywa katika mji wa Nagasaki, nchini Japan, kuadhimisha miaka 70 tangu kulipuliwa kwa bomu ya atomiki jijini humo.
Katika ibada hiyo mzee mmoja aliyenusurika aliibua hisia baada ya kukashifu hatua ya serikali iliyokomadarakani kwa kubadili vipengee vya katiba ya nchi hiyo ilikuruhusu wanajeshi wake kushiriki katika vita.
Manusura wa bomu hiyo ya Nyuklia iliyoua zaidi ya watu laki mbili
Maelfu ya watu waliohudhuria ibaada hiyo ya ukumbusho walimpigia makofi kwa uwazi wake.
Meya wa mji wa Nagasaki naye alivutia waya huohuo akimkashifu waziri mkuu bwana Shinzo Abe kwa jitihada za kubadilisha katiba ya nchi.
Wazungumzaji wamekashifu hatua ya serikali iliyokomadarakani kwa kubadili vipengee vya katiba ya nchi hiyo ilikuruhusu wanajeshi wake kushiriki katika vita.
Bwana Abe alikaa kimya kando tu jukwaani.
Bomu hilo lilidondoshwa na wanahewa wa Marekani, siku tatu tu baada ya kudondosha lingine la kinukilia katika jiji la Hiroshima.
Bomu hilo lilidondoshwa na wanahewa wa Marekani, siku tatu tu baada ya kudondosha lingine la kinukilia katika jiji la Hiroshima.
Bomu hilo liliangamiza kabisa mji huo na kuua watu zaidi ya 70,000 .
Inakisiwa kuwa zaidi ya watu 200,000 waliuawa katika milipuko hiyo miwili, na wengine kufariki baadaye kutokana na miale ya sumu kutoka kwa mabomu hayo ya nguvu za kitonaradi.

No comments:

Post a Comment