TANGAZO


Sunday, August 9, 2015

Maonesho ya Nane Nane mkoani Lindi

Wanafunzi wa shule ya Msingi Kitangali Mazoezi kutoka wilaya ya Newala Mkoani Mtwara wakipata maelezo juu ya masuala malimbali yanayohusu sera na huduma mbalimbali zinazotolewa na Wizara ya Fedha wakati wa Maonesho ya Kilimo ya Nane Nane kitaifa yanayoendelea uwanja wa Ngongo mkoani Lindi. 
Ofisa Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Mwajuma Msina akitoa maelezo kwa wageni waliotembelea banda la wizara hiyo wakati wa Maonesho ya Nane Nane kitaifa yanayoendelea katika uwanja wa Ngongo Mkoani Lindi.
Mtaalamu wa Mawasiliano kutoka Program ya Maboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (PFMRP) Wizara ya Fedha Alexander Iweikiza akitoa maelezo kwa wageni waliotembelea banda la wizara hiyo wakati wa Maonesho ya Nane Nane kitaifa yanayoendelea katika uwanja wa Ngongo Mkoani Lindi.  
Baadhi ya wageni waliotembelea banda la maonesho la Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) wakati wa Maonesho ya Nane Nane kitaifa yanayoendelea katika uwanja wa Ngongo Mkoani Lindi kujifunza namna wakala hiyo inavyotoa huduma kwa wananchi.
Mchumi kutoka Idara ya Bajeti ya Serikali Wizara ya Fedha Prosper Fivawo akitoa maelezo kwa mmoja wa wageni waliotembelea banda la wizara hiyo wakati wa Maonesho ya Nane Nane kitaifa yanayoendelea katika uwanja wa Ngongo Mkoani Lindi.  
Mtafiti wa kilimo kutoka taasisi ya Utafiti Kilimo Naliendele Festo Masisila akiwaeleza wakulima Thomas Mihambo (katikati) na Zuhura Nalipa (kulia) kutoka mtaa wa Mbawala Chini kata ya Naliendele mkoani Mtwara namna bora ya kulima zao la mhogo ikiwemo aina ya Kiroba, Pwani, Kizimbani, Makutupora, Dodoma, Mkumba na Mkuranga 1 inayostawi vizuri mkoani Mtwara wakati wa Maonesho ya Nane Nane kitaifa yanayoendelea katika uwanja wa Ngongo Mkoani Lindi. 
Ofisa Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Mwajuma Msina akiongea na wanafunzi wa shule ya Msingi Kitangali Mazoezi kutoka wilaya ya Newala Mkoani Mtwara kujua namna watoto wanavyonufaika na mfuko huo wakati wa Maonesho ya Nane Nane kitaifa yanayoendelea katika uwanja wa Ngongo Mkoani Lindi.
Mkazi wa kijiji cha Njenga Kata ya Ndanda wilaya ya Masasi mkoani Mtwara anayejishughulisha kujenga mitambo ya bio gas ambaye pia ni mkulima akiongea na wanachuo kutoka Chuo cha Ufundi (VETA) Lindi wakati wa Maonesho ya Nane Nane kitaifa yanayoendelea katika uwanja wa Ngongo Mkoani Lindi. 
Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Fedha wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya Msingi Kitangali Mazoezi kutoka wilaya ya Newala Mkoani Mtwara kujifunza masuala malimbali yanayohusu sera na huduma mbalimbali zinazotolewa na Wizara ya Fedha wakati wa Maonesho ya Kilimo ya Nane Nane kitaifa yanayoendelea uwanja wa Ngongo mkoani Lindi.(Picha zote na Eleuteri Mangi-MAELEZO, Lindi)

No comments:

Post a Comment