Waendesha mashtaka Sweden wanasema wametupilia mbali uchunguzi kufuatia tuhuma za unyanyasaji wa kingono dhidi ya mmiliki wa mtandao wa Wikileaks, Julian Assange, kwasababu wameishiwa na muda wa kuwasilisha mashtaka.
Lakini wataendelea kuchunguza tuhuma nyengine ya ubakaji.
Juliane Assange amekana mashtaka hayo.
Wakili wake, Per Samuelson, anasema mteja wake amevunjika moyo
"Hataki tuhuma ziondoshwe, anataka ajitakase.
Anaamini na mimi pia ninaamini kwamba iwapo mwendesha mashtaka atasikiliza upande wake wa kilichotokea wataelewa hana hatia na wataondosha tuhuma hizo kwa msingi kwamba hana hatia.
Kwa hivyo hii sio hali nzuri kwa Assange."
Mwanzilishi huyo wa Wikileaks amewalaumu upande wa mashtaka wa Sweden kwa kukataa kata kata kumsikiza.
Hata hivyo Assange amesalia katika ubalozi wa Ecuador mjini London tangu mwaka wa 2012 akihofia kushikwa na kuhamishwa hadi Marekani alikotakikana kwa kuchapisha habari za siri za serikali ya nchini hiyo.
Assange bado anakabiliwa na shtaka kuu la kunajisi.
No comments:
Post a Comment