Marufuku ya tambi za kampuni ya kutengeneza chakula ya Nestle imeondolewa.
Mahakama moja India imetoa uamuzi kwa manufaa ya kampuni ya kimataifa ya kutengeneza chakula Nestle kuhusu kupigwa marufuku tambi zake- Maggi.
Marufuku hiyo sasa imeondolewa kwa wiki sita kukisubiriwa ukaguzi mpya wa tambi hizo.
Nestle iliagizwa kuondosha tambi hizo za Maggi kutoka soko la India baada ya ukaguzi uliofanywa katika baadhi ya majimbo kugunduwa kuwa zina kiwango kikubwa cha madini ya Lead. Uamuzi huo unajri siku moja baada ya serikali ya India kusema inawasilisha kesi dhidi ya Nestle kutaka iilipe serikali takriban dola milioni mia moja kwa hasara.
No comments:
Post a Comment