Masoko ya sarafu duniani yamewekwa katika hali ya msukosuko kwa mara nyengine baada ya Uchina kuiruhusu thamani ya sarafu yake kushuka kwa siku ya pili mfululizo.
Lakini ni nini athari za kuanguka kwa sarafu hiyo kwa uchumi wa mataifa ya Afrika? Muhariri wa gazeti la Afrika Busines report Mathew David anafafanua.
Kuna madhara ya kawaida ya kushuka kwa sarafu hiyo kwani bei ya bidhaa zinazouzwa nje kutoka Uchina zitashuka huku bidhaa zinazouzwa kutoka bara la Afrika kwenda Uchina zikiwa ghali.
Lakini hilo litaziathiri bidhaa zilizotengezwa kwa kuwa bidhaa zinazouzwa na ambazo ndio nyingi kutoka barani Afrika huuzwa kwa kutumia sarafu ya dola.
Gavana wa benki ya Afrika Kusini amesema kuwa hali ya ushindani ya bidhaa zinazotengezwa nchini humo itaathirika,lakini akaongezea kwamba Afrika kusini haiuzi bidhaa nyingi kama hizo nchini Uchina.
Hatahivyo athari kubwa ni vile ambavyo Uchina ndio taifa linalofanya biashara na bara Afrika kwa wingi duniani.
Hatua hiyo inaamisha kwamba sarafu ya Yuan ina nguvu katika mataifa mengi barani Afrika.
Kwa mfano ,kwa sababu ya kiwango cha kibiashara kinachofanywa kati ya Kenya na Uchina na kiwango cha bidhaa za Uchina zinazoingia katika bandari ya Mombasa,serikali ya Kenya ina mpango wa kujenga kituo cha fedha za kigeni.
Vilevile sarafu ya Yuan inatumika katika uchumi ulio na sarafu nyingi wa taifa la Zimbabwe.
Lakini cha kuangazia zaidi ,miaka minne iliopita benki kuu ya Nigeria iliahidi kubadilisha na kuweka asilimia 5 hadi 10 ya fedha zake za kigeni zilizo katika hifadhi yake kama Yuan zikiwemo sarafu za dola na Yuro.
Kwa hivyo mataifa ya Bara la Afrika ambayo fedha zake zina uhusiano wa karibu na Uchina huenda fedha zao zikaathirika.
No comments:
Post a Comment