Andy Murray amefika raundi ya tatu katika kombe la Rodgers nchini Canada baada ya ushindi wa 6-4 7-5 mbele ya Mhispana Tommy Robredo.
Mchezaji huyo namba tatu kwa viwango vya tenisi duniani alitakiwa kucheza kwa siku ya pili baada ya mtanange wa kwanza uliochezwa siku ya jumanne kuvurugwa na mvua ambapo uliishia seti 4-4.
Mskochi huyo mwenye umri wa miaka 28 alipata maumivu katika mzunguko wa pili lakini alipata afueni na kumkabili Gilles Muller kutoka Luxembourg. ''Hali ilikua ngumu,upepo mkali, tofauti kabisa na ilivyokua jana.
Upepo ulipokua ukinikabili ilikua ngumu sana kuupata mpira'' alisema Murray.''Nilipoteza muelekeo kidogo katika mzunguko wa pili lakini niliimarika baadae.''
Kama Murray atafika fainali atachuana na Mswizi Roger Federer anayeshika nafasi ya pili katika viwango vya kimataifa.
No comments:
Post a Comment