Mratibu wa Trakoma toka hospitali ya KCMC Patrick Masae akifanya uchunguzi wa macho kwa wananchi wa kata ya Sinya na Tinga Tinga wilayani Longido.
Wanafunzi wa shule ya msingi sinya wakiwaonesha wageni (hawapo pichani) jinsi wanavyotumia kibuyu mchirizi kwa kunawa hii ni mojawapo wa mkakati wa usafi wa mazingira na kuimarisha usafi wa kunawa mikono na usi kutokomeza ugonjwa wa trakoma, upat.
Mratibu wa Trakoma toka Hospitali ya KCMC, Patrick Masae akimfanyia upasuaji mmoja wa wananchi wa Kata ya Sinya na Tinga Tinga, wilayani Longido.
Na Catherine Sungura,MoHSW
Sinya-Longido
WIZARA ya Afya na ustawi wa jamii itawafanyia upasuaji au urekibishaji wa vikope watu zaidi ya laki tano nchini hivi karibuni.
Sinya-Longido
WIZARA ya Afya na ustawi wa jamii itawafanyia upasuaji au urekibishaji wa vikope watu zaidi ya laki tano nchini hivi karibuni.
Hayo yamesemwa na mratibu wa kitaifa wa mpango wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Dkt.Upendo Mwingira kijijini hapa wakati aliwapokea wageni toka shirika lisilo la kiserikali la Ending Neglected Disease toka nchini Marekani.
Dkt. Mwingira alisema zoezi hilo la upasuaji limepangwa kufanyika mwezi wa kumi na litatekelezwa na halmashauri zenye kukabiriwa na wagonjwa wa Trakoma.
Aidha, alizitaja wilaya za longido,monduli na ngorongoro zinakabiliwa na wagonjwa wengi wa trakoma kutokana na ukame na mazingira waishiyo wananchi hao.
"inakadiliwa watu Wapatao laki moja nchini wanahitajika kufanyiwa urekibishaji wa vikope, na hii ni kutokana na takwimu za mwisho za mwaka 2014 toka utafiti huo kuanza mwaka 2004".
Alisema magonjwa haya yanahitaji kutokomezwa hapa nchini ili kuondoa upofu unaozuilika hivyo wizara inafanya zoezi kila mwaka la ugawaji wa dawa za' antibiotics ' kwa wananchi wote wa maeneo husika na kutumia kampeni ya SAFI ambayo ni kusafisha mazingira pamoja na kuimarisha upatikanaji wa maji safi kwa ajili ya kunawa uso ili kuzuia uenezwaji wa trakoma unaonezwa na mbu.
Awali mratibu wa mradi wa utafiti wa trakoma toka hospitali ya KCMC ambaye ndiye aliyekuwa akiwafanyia upasuaji wanakijiji hao Patrick Masae alisema changamoto kubwa inayowakabili wakati wa kuwafikia wananchi wenye matatizo hayo ni uelewa mdogo, hivyo kushindwa kujitokeza kufanyiwa upasuaji kwa wakati na hivyo kusababisha uharibifu wa kioo cha jicho na hivyo wanapofanyiwa upasuaji kwa kuchelewa huamini zoezi hilo si la kusababisha kuona.
No comments:
Post a Comment