MFAHAMU EMANUEL AUSTIN MTANZANIA MWANAMUZIKI AISHIYE UJERUMANI.
Emanuel Austin alizaliwa 27.10.1990 Jijini Dar es
salaam Tanzania, na ilipofika mwaka 1996
alihamia Ujerumani Kuishi na wazazi wake, Kipaji chake cha kucheza na
kuimba kilianza kuonekana mapema.
Akiwa na Miaka mitano Emanuel
Austin alianza kuigiza kama anacheza movie pamoja na rafiki zake wa Kiafrika
akiwemo Gregory Msuya na Michael Jackson.
Alipofika umri wa Miaka 15 alianza kupenda na kuimba muziki wa Kugani
yani ‘Hip hop’
Baadaye alitafuta baadhi ya
wenzake ambao aliona wanaweza kuingia studio na kufanya muziki wa Kughani yaani
Rap baadhi ya marafiki zake walikuwa ni pamoja na Miguel Amil Matos, Bernado
Ernest na Patrick Kitchens ambapo kwa Mara ya kwanza walifanya vizuri.
Mnamo mwaka 2002 wazazi wake
na Emanuel walianzisha Mradi mkubwa wa shule kwa ajili ya kufundisha Salsa huko
Großkrotzenburg jirani na Frankfurt , ambapo yeye binafsi alijifunza
Salsa na sasa amekuwa ni mwalimu mzuri wa Mtindo huo. Na kuanzia mwaka 2005
Emanuel na baba yake wamekuwa
wakiendesha programu ya kuwafundisha watoto salsa.
Kipaji cha nyota Mwanamuziki
Emanuel Austin kilianza kuonekana wakati ameanza kuimba Lebo ya MarciRecords
moja ya sehemu ambayo inawaunganisha wanamuziki mbalimbali na vijana ambao wanavipaji
katika sanaa ya Muziki, akiwa huko Emanuel alishinda tuzo ya Msanii
anayechipukia ndani ya Mji wa Hanau, Ujerumani
mwaka 2006.
Mwaka 2007 Emanuel alifanya
video yake ya kwanza kupitia wimbo wake wa Put your hands up wimbo uliotoka
katika album yake ya Put your Hands up, Album hiyo ilitengenezwa na Muandaaji
wa Muziki Dj Verde.
Mwaka 2008 Emanuel alifanya
ngoma nyengine ambapo alitoa audio pamoja na video , ngoma hiyo ilikwenda kwa
jina la Master of the Game, chini ya usimamizi wa mwandaaji wa Muziki Axel
Breitung hii ilikuwa ni nyimbo ambayo ilimuongezea umaarufu zaidi na kusikika
katika chanel maarufu za Televisheni kama VIVA na MTV.
Kutokana na mafanikio hayo
makubwa Emanuel alianza kuandaa matukio mbalimbali ikiwa ni pamoja na matamasha
ya muziki , Mwaka 2008 Emanuel aliamua kufungua darasa la mafunzo ambapo
ilikuwa ni Shule ya Muziki inayoitwa Tanzschule Weiss iliyopo Offenbach, ambapo
wanafundisha Hip hop, Kuwafundisha watoto kucheza na Salsa Cubana na anampango wa kuanzisha shule ya Muziki Nchini Tanzania.
Kwa sasa Emanuel Austin anafanya
kazi katika moja ya shule kubwa ya Muziki wa Dance nchini Ujerumani
ambapo wachezaji maarufu wa Dance kama Don Omar wapo humo , hata hivyo
Emanuel huja nyumbani Tanzania kila mwaka
na sasa Amekuja na ngoma mpya ambayo amemshirikisha Ben Pol inaitwa ruka
juu.
Kufahamu zaidi juu ya Emanuel Austin Mfuate hapa.
YouTube : Emanuel Austin
Twitter: emanuelaustin27
No comments:
Post a Comment