TANGAZO


Wednesday, July 1, 2015

Watia nia wa CCM waendelea kurejesha fomu za kuomba kuteuliwa na Chama

Dk. Hassy Kitine, akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kurejesha fomu zake kwa Naibu katibu Mkuu wa CCM Bara,  Rajab Luhavi za kuomba kuteuliwa na chama chake cha Mapinduzi (CCM), kuwania nafasi ya Urais katika Uchaguzi Mkuu ujao, mjini Dodoma leo. (Picha zote na John Banda)
Dk. Hamis Kigwangala akirejesha fomu kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rajab Luhavi Ofisi ya CCM Makao Makuu, mjini Dodoma leo.
Dk. Hamis Kigwangala, akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya kurejesha fomu kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rajab Luhavi Ofisi ya CCM Makao Makuu, Dodoma leo
Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa, akirejesha fomu kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rajab Luhavi Ofisi ya CCM Makao Makuu, Dodoma leo
Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa, akirejesha fomu kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara,  Rajab Luhavi Ofisi ya CCM Makao Makuu, Dodoma leo. 
Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Asha-Rose Migiro akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rajab Luhavi, wakati alipokwenda kurejesha fomu zake za kuomba kuteuliwa na chama hicho kwa nafasi ya Urais, Ofisi ya CCM Makao Makuu, mjini Dodoma leo.
Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Asha-Rose Migiro, akikabidhi fomu hizo kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rajab Luhavi, wakati akirejesha, Ofisi ya CCM Makao Makuu, mjini Dodoma leo.
Mkulima Eldifonce Bihole, akirejesha fomu zake za kuomba kuteuliwa na CCM kwa nafasi ya Urais.
Mtia nia Mpina, akizungumza na waandishi wa habari, wakati aliporejesha fomu za kuomba kuteuliwa kwa nafasi ya Urais na Chama chake cha CCM, mjini Dodoma leo.
Mwanafunzi wa Mzumbe Malik Salum Malupu, akizungumza na waandishi wa habari, wakati aliporejesha fomu zake za kuomba kuteuliwa kwa nafasi ya Urais na Chama chake cha CCM, mjini Dodoma leo.
Mwanafunzi wa Mzumbe Malik Salum Malupu, akizungumza na waandishi wa habari, wakati aliporejesha fomu zake za kuomba kuteuliwa kwa nafasi ya Urais na Chama chake cha CCM, mjini Dodoma leo.
Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba akirejesha fomu zake kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rajab Luhavi, Ofisi ya CCM Makao Makuu, mjini Dodoma leo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akirejesha fomu zake kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rajab Luhavi, Ofisi ya CCM Makao Makuu, mjini Dodoma leo.

No comments:

Post a Comment