Na John Banda, Dodoma
MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete leo amelizindua rasmi jengo la ukumbi wa mikutano la Chama hicho, mjini Dodoma.
Jengo hilo ambalo limezinduliwa leo, ndilo litakalotumika Julai 11 kwa ajili ya Mkutano Mkuu wa chama, utakaompata mgombea wake wa nafasi ya Urais, wa Tanzania na yule wa Zanzibar.
Rais Kikwete akieleza jambo alipokuwa akizungumza na wanaccm waliohudhuria katika uzinduzi wa jengo hilo jipya la ukumbi wa mikutano la chama hicho, mjini Dodoma leo.Jengo hilo ambalo limezinduliwa leo, ndilo litakalotumika Julai 11 kwa ajili ya Mkutano Mkuu wa chama, utakaompata mgombea wake wa nafasi ya Urais, wa Tanzania na yule wa Zanzibar.
Rais Kikwete akizungumza na wanaccm waliohudhuria katika uzinduzi wa jengo hilo jipya la mikutano la chama hicho, mjini Dodoma leo.
Rais Kikwete akielezea jambo, wakati akizungumza katika uzinduzi wa jengo hilo jipya la mikutano. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein na kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Rais Kikwete akimueleza jambo Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Rais Kikwete akikabidhiwa funguo na Balozi wa China nchini Tanzania, kama ishara ya kukabidhiwa jengo hilo kabla ya kulizindua rasmi leo.
Ukumbi wa mikutano unavyoonekana kwa ndani.
| Rais Kiwete akikagua ukumbi wa mikutano kwenye jengo hilo. |
| Jengo hilo linavyoonekana kwa nje. |
Jengo hilo linavyoonekana kwa nje.
Rais Kikwete akiwa ameshika funguo kuashiria kupokea rasmi jengo hilo baada ya kukabidhiwa na Balozi wa China nchini. Kulia ni aliyekuwa Balozi wa China nchini Tanzania, Dk. Li Yaqing na katikati ni Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein.
Rais Kikwete akikabidhiwa funguo na Balozi wa China nchini Tanzania, kama ishara ya kukabidhiwa jengo hilo kabla ya kulizindua rasmi leo. (Picha zote na John Banda)

No comments:
Post a Comment