Mjumbe wa Kamati iliyolenga kupata fedha
kwa ajili ya kuwasaidia wanahabari wanaougua magonjwa sugu (MEDIA CAR WASH FOR
CANCER) Wakili Aloyce Komba akiwaeleza waandishi wa habari mikakati ya usajili
wa umoja huo na taratibu za kuandaa katiba itakayoendesha umoja huo,wakati wa
mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Mjumbe wa Kamati hiyo Bi.
Leah Samike.
JUMLA ya shilingi milioni 31 zimepatikana katika harambee ya kuosha magari
iliyofanywa na waandishi wa habari Julai 4, 2015 katika viwanja vya Leaders
Club, Jijini Dar es Salaam. Kati ya fedha hizo, taslimu ni Milioni 12 na zingine
ni ahadi.
Harambee
hiyo inajulikana kwa jina la Media Car Wash for Cancer. Lengo la changizo hilo
lilikuwa kupata Shilinngi Milioni 100, ili kuwahudumia waandishi wenye matatizo
mbalimbali ya kiafya pamoja na kuwaingiza waandishi wa habari kwenye mfumo
rasmi Bima ya Afya.
Kama tulivyotanzaga awali, wagonjwa ambao ni
walengwa Adolf Simon Kivamo, Dastan
Bahai na Athumani Hamisi.
Ili
kutimiza lengo la changizo, Kamati ya Media Car Wash for Cancer inatarajia
kuendelea na zoezi la kutafuta pesa mpaka kiwango hicho kitakapofanikiwa.
Mpaka
sasa Kamati imeweza kuunda kamati ndogondogo zitakazosimamia zoezi la
ufuatiliaji na ukusanyaji fedha kulingana na ahadi mbalimbali na wataifanya
kazi hiyo kwa muda wa wiki moja.
Kisha,
wajumbe wa kamati hii ambayo jumla yao ni 75 watatoa maamuzi wa mgao huo mara
moja.
Kamati
hizo pia zitafanya kazi ya kuwatambua idadi ya kamili ya waandishi wengine
wanaosumbuliwa na magonjwa mbalimbali na hawana msaada unaoeleweka.
Aidha,
hali kadhalika, kamati hiyo pia inafanya tathimini ili kujua idadi ya
wanahabari ambao hawana Bima ya Afya ili utaratibu wa kuwaingiza kwenye mpango
huo uandaliwe.
Katika
awamu hii ya kwanza tunatarajia kuanza na wanahabari 50 ambao sio waajiriwa,
lakini wanafanya kazi katika vyombo vya habari nchini yaani Correspondents.
Uteuzi
wa majina ya waandishi utakwenda kwa kufuatana, yaani kutoka na chombo kimoja
hadi kingine.
Hii
ni mara ya kwanza katika historia ya Tanzania kwa waandishi wa Habari kuwa na
mfuko huu ambao lengo lake ni kwasaidia katika masuala ya matibabu.
Kamati
itaanza na waandishi wa habari walioko kwenye vyombo vya habari vya Jijini Dar
es Salaam na baadaye kuendelea katika mikoa mingine nchini.
Aidha,
Kamati ya Maandalizi ya Harambee hii imeitisha mkutano mkuu wa wadau wa habari
nchini utakaofanyika alhamisi Julai 16, 2015 kwa ajili ya kuanzisha mchakato wa
usajili wa chombo hiki muhimu.
Wahariri
wenu watakujulisheni muda na mahali utakapofanyika mkutano huu.
Pia,
kamati hii inakusudia kufanya harambee nyingine katikati ya mwezi Agosti mwaka
huu, itakayofanyika Jijini Mwanza.
Hatua
za awali za harambee hiyo kwa kushirikiana na wenzetu wa Jiji hilo
zimeanza,ikiwa ni pamoja na kutafuta eneo la kufanyia shughuli hiyo pamoja na
wadhamini mbalimbali.
Mwisho
tungependa kutoa shukrani zetu za dhati kwa wadhamini na wadau wote
walioshirikiana nasi katika harambee hii ambao ni BOT,TPB, NHIF, TANAPA, NSSF,
JUBILEE INSURANCE, ANSAF, ASTE INSURANCE, MOIL,TAGCO,TEA, Wizara Ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo,Bw. Reginald Mengi, Mh.Hamis Kagasheki, Mh.
Ridhiwani kikwete, Mh.Shabiby, Clouds FM, Radio Five,New Habari. The Guardian
Ltd, pamoja na Wanakamati,
Benjamin
Andongolile Thompson
Mwenyekiti
wa Kamati ya Maandalizi
Media
Campaign for Cancer Campaign



No comments:
Post a Comment