TANGAZO


Saturday, July 11, 2015

Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mjini Dodoma

Matukio ya mbalimbali katika picha ndani na nje ya ukumbi wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), mjini Dodoma leo.

Nasuala ya ulinzi uliimarishwa kuzunguka ukumbi wa mikutano wa CCM, ikiwemo Barabara kufungwa

Bernard Membe akikumbatiana na Januari Makamba baada ya kuingia katika Tano Bora, kabla ya kuchujwa na kubakia majina matatu tu ya John Magufuli, Asha-Rose Migiro na Amina Salim Ally.

Ulinzi ukiwa umeimarishwa baada ya kutokea ishara za fujo baada ya kukatwa jina la aliyekuwa mmoja wa wagombea wa nafasi hiyo, Edward Lowassa.
Askari wa Farasi akiimarisha ulinzi nje ya jengo la CCM, ili kudhibiti fujo baada ya kukatwa jina la aliyekuwa mmoja wa wagombea wa nafasi hiyo, Edward Lowassa.
Askari Polisi na wale wa Kutuliza Ghasia wakiimari ulinzi baada ya kutokea ishara za fujo baada ya kukatwa jina la aliyekuwa mmoja wa wagombea wa nafasi hiyo, Edward Lowassa.

Juu na Chini: Askari Polisi na wale wa Kutuliza Ghasia wakiimari ulinzi baada ya kutokea ishara za fujo baada ya kukatwa jina la aliyekuwa mmoja wa wagombea wa nafasi hiyo, Edward Lowassa.

Mwenyekiti wa CCM mkoani Shinyanga, Khamis Mgeja, akizungumza na waandishi wa habari.
Mwenyekiti wa CCM mkoani Shinyanga, Khamis Mgeja, akizungumza na waandishi wa habari.
Mashabiki wa Lowassa wakipaza sauti zao baada ya kukatwa jina la mgombea huyo.
Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete akiendesha mkutano huo. Kushoto ni Makamu wake kutoka Zanzibar, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein.
Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete (katikati), akituliza wajumbe katika mkutano huo. Kushoto ni Makamu wake kutoka Zanzibar, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein na kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Baadhi ya waliokuwa wagombea wa nafasi hiyo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazoro Nyalandu (katikati) na Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba (kulia), wakiwa nje ya ukumbi huo.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho (wa pili kulia), akiwa nje ya ukumbi wa mkutano.
Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete akifurahia jambo, wakati akiendesha mkutano huo. Kushoto ni Makamu wake kutoka Zanzibar, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein.
Mmoja wa wagombea, Edward Lowassa (kulia), akiteta jambo la mmoja wa kada wa chama hicho.
Msemaji wa CCM, Nape Nnauye, akimsalimia Mgombea liyekatwa, Edward Lowassa wakati wa kikao hicho.
Waandishi wa habari, wakimzonga mgombea liyekatwa, Edward Lowassa, ili aongee chocho. 
Askari Polisi na wale wa Kikosi cha Mbwa, wakiimari ulinzi nje ya jengo la mkutano huo.
Mmoja wa wagombea aliyekuwa ameingia Tano Bora na kisha jina lake kukwama kwenye tatu bora, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (kulia), akiteta jambo na mmoja wa kada wa CCM.
Mmoja wa wagombea wa nafasi hiyo, Asha-Rose Migira, akishuka kwenye gari lake kuelekea kwenye ukumbi wa mkutano huo.
Mmoja wa wagombea aliyekuwa ameingia Tano Bora na kisha jina lake kukwama kwenye tatu bora, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (kushoto), akiteta jambo na mke wa Rais, Mama Salma Kikwete.
Mmoja wa wagombea wa nafasi hiyo, William Ngeleja, akizungumza na waandishi wa habari.

Juu na Chini: Askari wakiweka hali ya ulinzi katika maeneo ya nje ya ukumbi wa mkutano huo.


Juu na Chini: Mashabiki wa wagombea wakipiga kelele za kulalamika katika maamuzi yaliyofanywa katika mkutano huo.



Mgombea aliyeingia katika Tatu Bora na mtarajiwa wa nafasi ya Urais kupitia CCM, John Magufuli, akifurahi baada ya kutangazwa kwenye tatu bora.



Wajumbe wakiwa katika mkutano huo.

Mashabiki wa wagombea wakipiga kelele.
Wajumbe wakiwa katika mkutano huo.
Gari la Polis likiwa Barabarani kuweka ulinzi nje ya jengo la CCM wakati wa mkutano huo. (Picha zote na John Banda, Dodoma)

No comments:

Post a Comment