PICHANI ni baadhi ya wakazi wanaodaiwa kuwa ni wavamizi katika eneo la Kijiji cha Ruvu Darajani, Kata ya Vigwaza Wilaya ya Bagamoyo, Mkoa wa Pwani, wakiwa wamejeruhiwa vibaya sehemu ya kichwani na mwilini kufuatia vurugu kubwa iliyotokea katika kijii hicho. Hapa wakiwa katika Zahanati ya kijiji hicho, wakakati huo, akiwemo Daktari mmoja ambaye wakati huo, alikuwa anamhudumia mmoja wa wajumbe wa Serikali ya kijiji Athumani Gereza ambaye alijeruhiwa vibaya sehemu ya kichwani. (Picha zote na Omary Said)
Mmoja wa wanaodaiwa kuwa wavamizi katika eneo la Kijiji cha Ruvu Darajani, Kata ya Vigwaza Wilaya ya Bagamoyo, Mkoa wa Pwani, akiwa hoi baada ya kujeruhiwa na kufikisha kwenye Zahanati ya kijiji hicho leo.
Na Omary Said, Ruvu
Julai 11
BAADA ya ya kuvutana kwa takribani zaidi ya miezi kadhaa sasa hatimae wakazi wa kijiji cha Ruvu Darajani, leo Julai 11 wamemwaga damu baada ya wakazi hao na wenzao wanaodaiwa kuingia katika eneo la kijiji hicho bila ridhaa ya kijiji kupigana mapanga.
Mbali ya hayo pia vibanda vilivyojengwa kwa kutimia udongo vilivyojengwa kwenye eneo hilo vimechomwa moto na vingine kuvunjwa hali iliyoongeza kuchochea ugomvi huo.
Chanzo cha kufikia hatua hiyo imetokana na mmoja wa wajumbe wa kijiji hicho Kamati ya ardhi Athumani Gereza kufika katika eneo lenye mgogoro kabla ya kuvamiwa na wakazi wanaodaiwa ni wavamizi na kuanza kumpiga na vitu mbalimbali hali iliyosababisha kupasuka sehemu ya kichwa hivyo kukimbizwa katika zahanati ya kijiji hicho kupatiwa huduma.
Mwandishi wa habari alifika zahanati na kumkuta mkazi huyo akiwa katika hali mbaya na hajitambui akishonwa sehemu ya kichwa huku hali yake ikiwa mbaya wakati ndugu na jamaa zake wakiangua vilio nje ya zahanati hiyo.
Wakizungumza kwa kukataa kutaja majina yao wakazi wa kijiji walisema kuwa hali hiyo imechochewa na serikali ya wilaya ya Bagamoyo mkoani hapa kwa kutochukua hatua mapema tangu sintofahamu hiyo lilivyoanza miezi kadhaa iliyopita.
Katika vulugu hiyo bali ya mjumbe huyo wa serikali ya kijiji kupasuliwa kichwani, pia wakazi wapatao sita wanaodaiwa kuwa ni wavamizi nao wamejeruhiwa vibaya sehemu za kichwa, usoni na maeneo mbalimbali huku wakiwa nje ya zahanati hiyo wakisubiri kupatiwa huduma.
“Kama unavyoona hali ni mbaya, sisi hatuwaonei huruma hawa watu sita sababu wao ndio chanzo cha leo kufikia hatua hii, wangekubalia maelekezo ya serikali ya kijiji cha Ruvu hali isingekuwa hivi, waache wasubiri mjumbe wetu wa kijiji Gereza apatiwe matibabu kwanza kwani hali yake ni mbaya,” walisikika wakazi hao.
Viongozi wa kijiji hawakuweza kupata muda wa kuzungumza na mwandishi kwani walikuwa katika harakati za kufika eneo la tukio linalodaiwa kuchomwa moto kwa vinanda hivyo hali ambayo iliwanyima kuzungumza na mwandishi.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Pwani Jafari Ibrahimu amethibitisha kutokea kwa fujo hizo na kueleza kwamba ulinzi zidi umeimarishwa katika kijiji hicho.

No comments:
Post a Comment