Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) Ndugu Jacqueline Maleko mara baada ya kuwasili kwenye sherehe za ufunguzi wa Maonesho ya Sabasaba kwenye Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam tarehe 3.7.2015.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa TANTRADE, Ndugu Edwin Rutageruka wakati alipowasili kwenye viwanja vya maonesho vya Mwalimu Julius Nyerere kuhudhuria sherehe za ufunguzi wa maonesho hayo uliofanya na Mheshimiwa Rais Dkt. Jakaya Kikwete tarehe 3.5.2015.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akikaribishwa na Mama Anna Mkapa kutembelea banda la Taasisi yake ya Fursa Sawa kwa wote (EOTF) mara baada ya Mheshimiwa Rais Dkt. Jakaya Kikwete kufungua rasmi maonesho hayo tarehe 3.7.2015.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiambatana na mwenyeji wake Mama Anna Mkapa wakiangalia bidhaa mbalimbali za akina mama wajasiriamali kutoka mikoa ya hapa nchini. Akina mama hao wanaratibiwa na Taasisi ya Fursa Sawa kwa Wote inayoongozwa na Mama Anna Mkapa.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, Mama Salma Kikwete akiwa na Mama Anna Mkapa wakifurahia bidhaa za vikapu zilizotengenezwa na akina mama wajasiriamali kutoka mkoani Singida kwenye Maonesho ya Sabasaba yanayofanyika Dar es Salaam.
Mke wa Rais
Mama Salma Kikwete akipata maelezo ya bidhaa mbalimbali za asili wakati
alipotembelea banda la Fursa Sawa Kwa Wote kwenye Maonesho ya Sabasaba tarehe
3.7.2015. Kulia kwa Mama Salma ni Mama Anna Mkapa akifuatiwa na Mkuu wa Wilaya
ya Temeke Ndugu Sophia Mjema.
No comments:
Post a Comment