TANGAZO


Wednesday, July 29, 2015

Jaji Mutungi ajiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapigakura

ZIKIWA  zimebakia siku chache tu kuisha kwa siku zilizotengwa na Serikali kwa wananchi kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura kwa mfumo wa BVR katika Jiji la Dar es Salaam.
Mwandikishaji Msaidizi Bi. Maida Ally Yusufu akimsainisha Jaji Mutungi  fomu ambazo zimebeba taarifa zake kwa ajili ya kujiandikisha Leo katika kituo cha Shule ya Msingi Bunge Jijini Dar es Salaam.
Alama za vidole zikichukuliwa na Mwandikishaji Bw. Ernest Moses Selelya mara baada ya kukamilisha taratibu za ujazaji wa fomu ya utambulisho. 
Mhe. Jaji Francis Mutungi akipigwa picha kwa ajili ya kupata kadi ya mpiga kura, wakati alipokwenda kujiandikisha leo.
Mhe. Jaji  Francis Mutungi akipokea  kitambulisho cha mpiga kura kutoka kwa Mwandikishaji Bw. Ernest Moses Selelya.
Mhe. Jaji Francis S. K. Mutungi akiwa na kitambulisho chake mara baada ya kujiandikisha mapema Leo katika kituo cha Shule ya Msingi Bunge Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment