TANGAZO


Sunday, July 19, 2015

Burundi:Mazungumzo ya amani yakwama

Mazungumzo ya amani nchini Burundi
Mazungumzo ya mwisho ya kuzima msukosuko wa kisiasa wa Burundi, yamesimamishwa, siku mbili kabla ya uchaguzi wa rais.
Waziri wa mambo ya ndani wa Burundi, ameripotiwa akisema, kuwa mpatanishi mkuu, yaani Uganda, imeombwa iruhusu mazungumzo yasimamishwe baina ya serikali ya Burundi na vyama vya upinzani.
Pande zote mbili zinalaumiana kwamba hazionyeshi nia njema kwenye mazungumzo.
Upinzani umesema utasusia uchaguzi huo, ambapo rais Pierre Nkurunziza anawania muhula wa tatu hatua ambayo inaonekana na wengi kuwa kinyume na katiba.
Hatua hiyo ilizua maandamano ya majuma kadhaa na jaribio la mapinduzi awali mwaka huu.

No comments:

Post a Comment