TANGAZO


Thursday, July 9, 2015

Athari ya madini ya Zebaki katika mwili wa binadamu

Mwakilishi wa Taasisi ya Umoja wa Mataifa ya Mafunzo na Utafiti(UNITAR), Carlos Maren (kushoto) akitoa hotuba yake  wakati wa mkutano wa  Mkataba wa  Minamata kuhusu  madini ya zebaki uliofanyika jana kwenye hoteli ya Peacock  jijini Dares Salaam.(Katikati) ni  Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya  Makamu wa Rais Anjelina Madete  na  Kulia ni Mkurugenzi wa Mazingira kutoka ofisi hiyo, Joseph Kihaule. 
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya  Makamu wa Rais Anjelina Madete (katikati) akifungua mkutano wa  Mkataba wa  Minamata kuhusu  madini ya zebaki uliofanyika jana kwenye hoteli ya Peacock  jijini Dares Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Mazingira kutoka ofisi hiyo, Joseph Kihaule na  kushotoni Mwakilishi wa Taasisi ya Umoja wa Mataifa ya Mafunzo na Utafiti(UNITAR), Carlos Maren. 
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya  Makamu wa Rais Anjelina Madete(katikati) akifungua mkutano wa  Mkataba wa  Minamata kuhusu  madini ya zebaki uliofanyika jana kwenye hoteli ya Peacock  jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Mazingira kutoka ofisi hiyo, Joseph Kihaule na  kushotoni Mwakilishi wa Taasisi ya Umoja wa Mataifa ya Mafunzo na Utafiti(UNITAR), Carlos Maren. 
Picha ya pamoja kati ya Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Anjelina Madete (wa pili kushoto)  mara baada ya kufungua mkutano wa  Mkataba wa  Minamata kuhusu  madini ya zebaki uliofanyika jana kwenye hoteli ya Peacock  jijini Dares Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Mazingira kutoka ofisi hiyo, Joseph Kihaule na  (wa pili kulia) ni  Mwakilishi wa Taasisi ya Umoja wa Mataifa ya Mafunzo na Utafiti (UNITAR), Carlos Maren. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa mazingira kutoka ofisi hiyo, Rogathe Kisanga. 
Issaria Mangalili akitoa mada juu ya mikataba mbalimbali inayohusu kemikali mkutano wa Mkataba wa  Minamata kuhusu  madini ya zebaki uliofanyika jana kwenye hoteli ya Peacock  jijini Dares Salaam. 
Issaria Mangalili akitoa mada juu ya mikataba mbalimbali inayohusu kemikali mkutano wa Mkataba wa  Minamata kuhusu  madini ya zebaki uliofanyika jana kwenye hoteli ya Peacock  jijini Dares Salaam. 
Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Joseph Kihaule (kushoto) akisisitiza jambo wakati akiongoza mkutano wa Mkataba wa Minamata kuhusu  madini ya zebaki uliofanyika jana kwenye hoteli ya Peacock  jijini Dares Salaam, kulia ni Mwakilishi wa Taasisi ya Umoja wa Mataifa ya Mafunzo na Utafiti(UNITAR), Carlos Maren. 
Wadau wa mkutano wa  Mkataba wa  Minamata kuhusu  madini ya zebaki uliofanyika jana wakijadiliana  jambo  kwenye hoteli ya Peacock  jijini Dares Salaam. 
Mdau wa mkutano wa  Mkataba wa  Minamata kuhusu  madini ya Zebeki uliofanyika jana kwenye hoteli ya peacock  jijini Dares Salaam, Anne Sekiete ,ambaye ni Afisa Afya Mkuu kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii akichangia   jambo. Picha zote na Magreth Kinabo – Maelezo

Na Magreth Kinabo- Maelezo
JAMII imelezwa kwamba ulaji wa samaki wakubwa na vyakula vya jamii  hiyo(shellfish),ambao wameathirika madini ya zebaki kwa wingi unasababisha binadamu kupata madhara  ya kiafya kutokana na baadhi ya samaki hao kula samaki wadogo wenye madini hayo.
Samaki hao huathirika na madini hayo kutokana na shughuli za mlipuko wa volkano, mmomonyoko wa ardhi,  na shughuli za kibinadamu ambazo ni uchimbaji mdogo  wa madini,uchomaji wa mkaa, uzalishaji wa saruji.
Hayo yalisemwa jana na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi.  Anjelina Madete wakati  akifungua Mkutano wa  Mkataba wa  Minamata kuhusu  madini ya zebaki, ambayo ulijadili juu ya mbinu za utekelezaji  wake ili kuweza kuepusha madhara kwa jamii  uliofanyika jana kwenye hoteli ya Peacock  jijini Dares Salaam.

“Watu huathiriwa na madini haya katika mazingira tofauti, ingawa huathiriwa zaidi kutokana ulaji wa samaki ambao wana madini haya na pia kwa kuvuta hewa yenye madini haya kutokana na shughuli za  viwandani,” alisema.

Aliyataja makundi ambayo ni rahisi kupata madhara ya madini hayo kuwa ni watoto wachanga ambao hawajazaliwa kutokana mama zao kutumia vyakula vya  jamii hiyo, hali inayosababisha kuathiri ukuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu  kwa watoto, hivyo huathiri uwezo wa kufikiri, kumbukumbu , uelewa,  kuwa na umbo dogo na uwezo wa kuona.

Aliongeza kuwa, kundi la pili  linaloathirika kuwepo kwa madini hayo kwa wingi ni jamii inayoishi kwa kutegemea samaki  uchunguzi umeonyesha 1.5/1000 na 17/1000 watoto waliopata upungufu wa akili kutokana  na matumizi ya samaki wenye madini hayo katika nchi za Brazil ,Canada, China, Columbia na nchi za ukanda wa kijani.

Naibu Katibu Mkuu huyo pia aliyataja  madhara yanayotokana na kuwepo kwa madini ya zebaki  mwilini kwa wingi ni huathiri kwa mfumo wa fahamu, usagaji wa chakula, kinga za mwili mapafu, figo, ngozi na macho.

Alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizosaini Mkataba huo Oktoba 10 nchini Japan mwaka 2013. Hivyo elimu inahitajika kwa jamii juu madini hayo ikiwemo kujenga uwezo wa rasilimali watu, miundombinu na mahitaji mengine kwa ajili ya usimamizi na ufuatiliaji wa upunguzaji wa madini  hayo.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Taasisi ya Umoja wa Mataifa ya Mafunzo na Utafiti(UNITAR), Carlos Maren alisema wamefurahishwa na kitendo cha Tanzania kuweka mikakati ya utekelezaji wa mkataba huo ili kuokoa maisha ya watu, hivyo wataendelea kutoa ushirikiano.

No comments:

Post a Comment