*Sasa iko hewani
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Assah Mwambene, akizungumza jamabo.Hussein Makame-MAELEZO
WIZARA ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kupitia Idara ya Habari- MAELEZO, imekamilisha kazi ya kuboresha Tovuti ya Wananchi na sasa iko hewani.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za Wizara hiyo, Mkurugenzi wa MAELEZO Assah Mwambene, aliwataka wananchi kuitumia tovuti hiyo kupitia anuani ya HYPERLINK "http://www.wananchi.go.tz" www.wananchi.go.tz kuwasilisha hoja zao Serikalini ili ziweze kupatiwa majibu.
“Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kupitia Idara ya Habari- MAELEZO, imekamilisha kufanya maboresho ya tovuti ijulikanayo kwa jina la Tovuti ya Wananchi” alisema Mwambene na kuongeza:
“Lengo letu sasa ni kutaka wananchi badala ya kuhangaika sana, akiwa sehemu yoyote ya nchi hii anaweza kuuliza swali kupitia mtandao wa intaneti kwa anuani ya HYPERLINK "http://www.wananchi.go.tz" www.wananchi.go.tz ”
Alisema mwananchi akiingia kwenye tovuti hiyo atakutana na sehemu ya kuweka hoja yake kuuliza swali, kutoa maoni, kutoa pongezi, kuwasilisha malalamiko yake na moja kwa moja yatapokelewa na MAELEZO na kufanyiwa kazi.
“Mwananchi anaweza kuandika swali moja kwa moja kwenye taasisi anayotaka swali lile liende, kwa mfano kama anataka swali lile liende Wizara ya Ardhi anaweza akaandika” alisema Mwambene na kuongeza:
“Sisi tutapata taarifa kwamba ameleta swali na tutalipeleka kwenye taasisi husika na tutaangalia na kuona je swali hilo limejibiwa ama halijajibiwa”.
Mwambene alifafanua kuwa kila siku MAELEZO itajua ni wizara gani ama taasisi gani ya Serikali imepelekewa swali gani na swali hilo limejibiwa au la.
Alisema tovuti hiyo ni chombo muhimu katika mabadiliko ya sayansi na teknolojia na itamfanya mwananchi asilazimike kutembea kutoka kwenda wizara moja hadi nyingne ama taasisi ya Serikali kushughulikia malalamiko yake.
Alitoa mfano kuwa hata mwananchi akitaka kujua jinsi ya kupata viza au huduma nyingine inayotolewa na Serikali ataweza kupatiwa majibu ndani ya muda mfupi sana kupitia tovuti hiyo ya Wananchi.
“Baadaye kuna jambo lingine ambalo bado tunalifanyia tathimini, ni suala la kwamba wanaanchi wanaweza kutumia simu zao za mkononi kutuma maswali na kupokea majibu” alisema Mwambene.
Alibainisha kuwa tathimini hiyo ikikamilika hivi karibuni, watatoa namba ambayo mwananchi anaweza kutumia ujumbe mfupi wa simu ya mokononi kutuma hoja yake Serikalini na kupatiwa majibu kupitia njia hiyo.
“Ni tovuti ambayo tunapenda wananchi waitumie ili kupunguza gharama na muda mwingi sana kwa mfano mtu kusafiri, kupanda gari kwenda wizarani au taasisi ya umma kufuatilia shida yake.Hivyo anaweza kutumia simu yake ya mkononi” alisema Mwambene na kuongeza:
“Lengo letu ni kwamba wananchi waone kama hiyo ni fursa muhimu ya mawasiliano na waone kuwa sasa hivi wanaweza kutuandikia ujumbe kuuliza swali au malalamiko na yatatufikia na kufanyiwa kazi”.
Mwambene alisema Wizara imejipanga vya kutosha kuhakikisha kwamba Serikali inawasiliana na wananchi wake kwa kusikiliza shida zao na kuzipatia majibu.
“Hii ni Serikali ya wananchi na lazima tuwasiliane na wananchi kwa njia yoyote ambayo ni rahisi kuwafikia na Serikali imeona hii ni njia rahisi zaidi kuwafikia kupitia mtandao huu wa Tovuti ya Wananchi” alisema.
Tovuti ya Wananchi imewahi kufanya kazi katika miaka iliyopita na baadaye ilisimama lakini sasa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imeifanyia marekebisho makubwa na iko hewani.
No comments:
Post a Comment