Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa Ndugu Juma
Khatib Chum akifungua mradi wa maji wa Kijiji cha Kibedya Wilayani Gairo
Na Andrew Chimesela
0719
11 22 99/0785 336 335
(16
Juni, 2015)
MWENGE wa uhuru ambao kwa
sasa uko Mkoani Morogoro, umepitia miradi mbalimbali ya maendeleo ukiwemo mradi
wa maji uliogharimu shilingi 555,227,710.40
na unatazamiwa kuwapatia maji safi na salama wananchi 10,534 ambao ni wakazi wa kijiji cha
Kibedya Wilayani Gairo.
Mwenge huo ambao umeingia
siku yake ya pili, tangu kuwasili Mkoani
Morogoro ukitokea Mkoani Tanga, na kukimbizwa Wilaya ya Mvomero, Leo ukiwa
Wilayani Gairo umefungua mradi wa maji wenye matenki mawili yenye jumla ya lita
za ujazo 180,000.
Kwa mujibu wa maelezo
yaliyotolewa kwa Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Bw. Juma Khatib Chum, muda
mfupi kabla kuufungua, ilielezwa kuwa mradi wa maji wa Kibedya uliibuliwa na
wananchi na kuingizwa kwenye program ya Serikali ya miradi ya maji ya vijiji
kumi Wilayani Gairo.
Mradi wa Maji wa Kibedya
umejengwa kwa ufadhili wa Benki ya Dunia kupitia mpango wa maendeleo ya Sekta
ya Maji, na wananchi kuchangia ardhi ulipojengwa mradi huo yenye thamani
ya shilingi 1,500,000,.00.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa
lengo mahsusa la mradi huo ni kuwapatia wananchi wa Kijiji cha Kibedya maji
safi na salama hali itakayochangia kuboresha maisha yao kwa kupata muda wa
kutosha kufanya shughuli nyingine za kiuchumi badala ya kutumia muda huo
kutafuta maji.
Naye Kiongozi wa Mbio za
Mwenge Kitaifa Juma Khatib Chum baada ya kuufungua, mradi huo, aliwataka
wananchi wa Kijiji cha kibedya kuuendeleza na kuutunza mradi huo ili uweze
kudumu kwa muda mrefu.
“ Ninawasihi wananchi wa
Kijiji cha Kibedya kuendeleza na kutunza
miundombinu ya mradi huu pamoja na vyanzo vyake vya maji ili mradi udumu kwa
muda mrefu na kuja kunufaisha vizazi vingine vijavyo” alisema.
Mwenge wa uhuru leo
umekimbizwa katika Wilaya ya Gairo ambapo umepitia jumla ya miradi ya maendeleo
sita, yenye thamani ya shilingi, 905,071,355.40.
Hiyo ikiwa ni pamoja na
mchanggo kutoka Serikali Kuu ni shilingi 715,390,635.40, mchango kutoka Halmashauri
ya Gairo shilingi 7,578,720.00, nguvu za wananchi silingi 180,387,000.00 na
wahisani walichangia shilingi 1,715,000.00.
Mwenge wa Uhuru kesho utakimbizwa
katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.
No comments:
Post a Comment