Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Biashara ya DCB, Balozi Paul Rupia akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa filamu ya Desire to Succeed juzi jijini Dar es Salaam.Filamu hiyo imetengenezwa na ya Kampuni ya Consnet Group Ltd ya jijini Dar es Salaam kufuatia udhamini wa DCB Benki ikiwa ni njia ya kujitangaza.
Mwakilishi wa Kampuni ya Consnet Group ambayo ndiyo waandaaji wa filamu ya Desire to Succeed Bw. Sanctus Mtisimbe (mwenye tai nyekundu) akiwatambulisha baadhi ya wasanii (wahusika) muhimu walioshiriki katika filamu hiyo juzi jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa filamu hiyo iliyoambatana na futari chini ya udhamini wa Benki ya Biashara ya DCB.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo akitambulishwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa filamu ya Desire to Succeed iliyodhaminiwa na benki hiyo kwa lengo la kuhamasisha jamii kutumia huduma za kibenki katika kuyafikia mafanikio yao.
Baadhi ya wasanii waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa filamu ya Desire to Succeed wakijitambulisha juzi jijini Dar es Salaam.Filamu hiyo iliyodhaminiwa na benki ya Biashara ya DCB.
Kutoka kushoto ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya
Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo, msanii Rose Ndauka, Tito Mrisho Zimbwe na
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Biashara ya DCB Balozi Paul Rupia
wakionyesha DVD ya filamu ya Desire to Succeed juzi jijini Dar es Salaam mara baada
ya kuzinduliwa rasmi. Filamu hiyo imetengezwa na kampuni ya Consnet Group chini
ya udhamini wa DCB Benki ikiwa ni njia ya kujitangaza kupitia ubunifu wa sanaa
ya filamu.
Na Frank Shija, WHVUM
BODI ya Filamu Tanzania imepongeza kwa juhudi zake za kuendeleza na kusaidia kukua
kwa tasnia ya filamu nchini.
Pongezi
hizo zimetolewa juzi jijini Dar es Salaam na Balozi Paul Rupia alipokuwa mgeni
rasmi katika hafla ya uzinduzi wa Filamu ya Desire to Succeed.
Balozi
Rupia alisema kuwa tasnia ya filamu inazid kukua nchini sambamba na kuongezeka
kwa wasanii kuzingatia maadili ya Kitanzania.
Niseme
wazi tu kwamba Serikali kupitia Bodi ya
Filamu nchini inafanya kazi thabiti tofauti na ilivyokuwa huko nyuma ambapo
watendaji wa Bodi hiyo walikuwa na kazi ya kukagua tu tofauti na sasa wanatoka
na kuhamasisha ukuaji wa tasnia hii” Alisema Balozi Rupia.
Aidha
Balozi Rupia ametoa rai kwa taasisi za umma na binafsi kutambua mchango wa
wasanii na kuwatumia vyema katika program zao za kujitangaza ndani na nje ya
nchi kama ambayvo DCB benki ilivyotumia fursa hiyo.
Kwa
upande wake Mwakilishi wa Kampuni ya Consnet Group Bw. Sanctus Mtsimbe amesema
kuwa imekuwa ni faraja kwa wasanii kuona kuwa kazi zao na mchango wao katika
jamii unatambuliwa na baadhi ya taasisi hapa nchini na kuongeza kuwa hiyo
inaonyesha dalili njema katika ukuaji wa tasnia ya filamu.
Aliongeza
kuwa katika filamu ya hiyo ya Desire to Succeed wasanii wameitendea haki kazi
yao na kwa kuzingatia matakwa ya kanuni na maelekezo ya Bodi ya Filamu Tanzania
ikiwa ni pamoja na kuzingatia mavazi yenye staha kwa mujibu wa maadili ya
kitanzania.
Mtsimbe
ametoa rai kwa wadau wa tasnia ya filamu kununua nakala za filamu hiyo ambayo
itapatikana madukani kwa bei ya shilingi 3000/= ili wajionee namna kazi nzuri
ya wasinii wetu.
Filamu
ya Desire to Suicceed ni filamu ya kwanza nchini Tanzania ambayo maudhui yake
yamekuwa na malengo makuu mawili kwa wakati mmoja ikiwa ni kuelimisha na
matangazo ya biashara kwa wahusika kutumia Bidhaa za Benki ya DCB katika
kuuisha hadithi yao. DCB Benki ndiyo mthamini wa filamu hiyo ambaoyo
imetengenezwa na Kapmuni ya Consnet Group huku ikishirikishwa wasanii Tito Mrisho
Zimbwe (Muhusika Mkuu), Rose Ndauka,Jackline Pentezel, Hidaya Njiadi, Gojak na
wengine.
No comments:
Post a Comment