TANGAZO


Saturday, June 27, 2015

Ghana FA lakanusha ubadhirifu Brazil

Ghana FA lakanusha ubadhirifu Brazil
Shirikisho la soka la Ghana GFA limekanusha madai ya ubadhirifu wa fedha katika kombe la dunia la Brazil 2014.
Shirikisho hilo limeitupia tope ripoti ya kamati maalum iliyoundwa kutathmini sababu za matokeo duni huko Brazil 2014.
''Kamati ya Dzamefe'' ilichapisha ripoti yake majuzi na ikaonesha kuwa mpakuaji mipira wa timu ya Black Stars alilipwa kiasi sawa cha fedha na Washambuliaji Asamoah Gyan na hata kocha wa timu ya taifa James Kwesi Appiah.
null
Meza ya michezo ya BBC ndiyo iliyopasua mbarika kuwa Hamidu alilipwa pesa sawa na kocha na wachezaji nyota .
Ripoti hiyo ilionesha kuwa yule msaidizi anayeokota mipira na kupanga jezi za timu ya taifa alilipwa takriban dola laki moja $100,000.
Ismail Hamidu alipokea pesa hizo japo GFA inailaumu kamati hiyo kwa kuidunisha kazi yake.
Meza ya michezo ya BBC ndiyo iliyopasua mbarika kuwa Hamidu alilipwa pesa sawa na kocha na wachezaji nyota .
null
Sasa GFA imewataka mawakili wake wawasilishe kesi mahakamani kupinga kuchafuliwa jina
Kamati hiyo vilevile inasema kuwa kunakiasi kikubwa tu cha pesa zilizopewa GFA ambazo hazijabainika zilipo.
Sasa GFA imewataka mawakili wake wawasilishe kesi mahakamani kupinga kuchafuliwa jina.
Ghana ilishindwa kufuzu kwa mkondo wa pili huko Brazil licha ya serikali kutuma zaidi ya dola milioni 3 pesa taslimu kupelekwa Brazil ilikuzima mgomo wa wachezaji waliokuwa wakilalamikia malimbikizi ya marupurupu yao.

No comments:

Post a Comment