TANGAZO


Monday, June 15, 2015

Sheikh Mkuu wa Tanzania na Kiongozi wa Bakwata, Mufti Shaaba Issa Bin Simba afariki dunia

Mufti Sheikh Shaaban Issa Bin Simba

Na Kassim Mbarouk
SHEIKH Mkuu na Kiongozi wa Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata), Mufti Sheikh Shaaban Issa Bin Simba amefariki duni leo baada ya kuugua na kulazwa Hospitali ya TMJ, Masaki jijini Dar es Salaam, kutokana na maradhi ya kisukari yaliyokuwa yakimsumbua kwa muda mrefu sasa.

Kutokana na ratiba ya mazishi iliyotolewa na familia yake, mwili wa Mufti kesho asubuhi utasafirishwa kwa ndege kutoka Dar es Salaam kuelekea nyumbani kwao, Shinyanga kwa mazishi yatakayofanyika hiyo hiyo kesho.

Watu binafsi, Taasisi, Mashirika mbalimbali ya Serikali na ya watu binafsi pamoja na Wizara mbalimbali za wametoa rambirambi zao na kumwelezea Mufti kuwa alikuwa mtu aliyekuwa mwelevu na msikivu kwa Waumini aliokuwa akiwaongoza na Watanzania kwa ujumla.

Na kusema kuwa ameacha pengo lisiloweza kuzibika kirahisi. 

No comments:

Post a Comment