TANGAZO


Monday, June 15, 2015

Profesa Lipumba alivyochukua fomu ya kuomba kuteuliwa na Chama chake cha CUF kuwania nafasi ya Urais

Wanachama wa Chama cha Wananchi (CUF), wakiwa kwenye gari, maeneo ya Ubungo Riverside, wakielekea ukumbi wa Hoteli ya Blue Pearl kumsindikiza Mwenyekiti wao, Profesa Ibrahim Lipumba, kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa na chama kwa ajili ya nafasi ya Urais, Dar es Salaam jana. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)




Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, akionesha fomu ya kuomba ridhaa ya chama chake kumteua kuwania nafasi ya urais, mara baada ya kukabidhiwa na Katibu wa CUF, Wilaya ya Kinondoni, Mohamed Mkandu (kulia), Dar es Salaam jana. 





Wanachama wa Chama cha Wananchi (CUF), wakishangilia wakati Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba, alipokuwa akizungumza nao mara baada ya kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya chama chake, kuwania nafasi ya Urais, Dar es Salaam jana. 

















 Msanii wa vichekesho Ismail Makombe 'Baba Kundambanda', akichekesha wakati wa mkutano wa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF),Profesa Ibrahim Lipumba (kushoto), kuchua fomu ya kuomba ridhaa ya chama chake kuwania nafasi ya Urais, Dar es Salaam jana. Katikati ni Katibu Mkuu wa CUF, Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad. 















Profesa Lipumba akiwaaga wanachama na mashabiki wa chama hicho, wakati akiondoka ukumbini baada ya kuwahutubia jana.

No comments:

Post a Comment