Serikali ya Kenya imeondoa marufuku dhidi ya kampuni za kupokea na kuhamisha fedha maarufu Hawala zinazotumiwa na raia wengi wa Somalia.
Benki kuu ya Kenya imeandikia moja kati ya kampuni hizo ,kuthibitisha kwamba marufuku hiyo imeondolewa.
Wiki iliopita ,rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alisema kuwa aliiagiza benki kuu kuondoa marufuku hiyo na kuweka mipango mipya itakayofuatwa na kampuni hizo wakati wanapotumia mpango huo wa fedha.
Serikali ilizipiga marufuku kampuni 13 za Hawala mnamo mwezi Aprili kufuatia mauaji ya watu 148 katika chuo kikuu cha Garissa na wapiganaji wa kundi la Alshaabab.
Serikali inasema kuwa marufuku hiyo inalenga kuwazuia wapiganaji wa kiislamu kutotumia kampuni hizo kufanya oparesheni zake.
Marufuku hiyo ilizua hisia kali kutoka kwa raia wa Somalia ambao wameishtumu serikali kwa kutoa adhabu ya jumla.
No comments:
Post a Comment