Ripoti iliyosubiriwa na wengi, imeonyesha kuwepo na ushahidi wa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu pamoja na sheria ya kimataifa kutoka kwa pande zote.
Israel imepuzilia mbali ripoti hiyo na kuitaja kama inayochochewa kisiasa.
Vita hivyo vilisalia kwa siku 50 na kumalizika kwa mkataba wa amani.
Kwa upande wa Palestina watu 2,251, zaidi ya elfu moja wakiwa ni raia waliuawa.
Upande wa Israel uliwapoteza wanajeshi 67 wakiwemo raia sita.
Israel imejitetea na kusema ilianzisha operesheni dhidi ya Gaza ili kuzima mashambulio ya roketi yaliyokua yakirushwa na makundi ya wapiganaji, ambayo yalichimba mahandaki kutekeleza mashambulizi.
Ripoti hii ya tume ya haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa ilikumbwa na mzozo tangu mwanzo.
Mkuu wa uchunguzi alilazimika kujiondoa bada ya Israel kulalamika kwamba alikuwa na uwonevu.
Aidha alituhumiwa kuwahi kufanya kazi na chama cha ukombozi wa Palestina PLO.
Israel ilikataa kushirikiana na uchunguzi kwa madai kwamba tayari ilikua imehukumiwa tangu mwanzo.
No comments:
Post a Comment