Tuesday, June 2, 2015
Serikali yamaliza mgogoro na wafanyabiashara
Waziri wa Fedha Mh. Saada Mkuya Salum akiwaeleza wafanya biashara kuendelea kutoa ushirikiano, utakaojenga uhusiano wa kudumu kati yao na Serikali kwa maslahi na maendeleo ya Taifa, wakati akitoa Taarifa ya muafaka uliofikiwa kati ya wafanyabiashara na serikali juu ya Matumizi ya Mashine za kielektroniki (EFDs) leo Jijini Dar es Salaam.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Rished Bade akimshukuru Waziri wa Fedha kwa ushirikiano wanaoendelea kuuonyesha kwa mamlaka hiyo hasa katika kukabiliana na changamoto mbalimbali katika suala la ukusanyaji Kodi nchini.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabishara Bw. Johnson Minja akimueleza Waziri wa Fedha Mh. Saada Mkuya Salum kuridhishwa na utendaji wa Serikali katika utatuzi wa changamoto za wafanyabiashara na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano ili kwa pamoja waweze kufikia malengo ya taifa ya kuwa na uchumi imara kupitia ukusanyaji wa Kodi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mzee Benard Mchovu akipongeza kazi iliyofanywa Kamati ya uhamasishaji wa matumizi ya mashine za kielektroniki (EFDs) na kuwaasa kuendelea kutoa ushirikiano kwa maslahi ya Taifa kwa Ujumla.
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya Salum akiwa katika picha ya pamoja wafanyabiashara alipotoa taarifa ya muafaka uliofikiwa kati ya wafanyabiashara na Serikali juu ya Matumizi ya Mashine za kielektroniki (EFDs) leo, Jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabishara Bw. Johnson Minja na Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mzee Benard Mchovu.
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya Salum akiwa katika picha ya pamoja wafanyabiashara alipotoa taarifa ya muafaka uliofikiwa kati ya wafanyabiashara na Serikali juu ya Matumizi ya Mashine za kielektroniki (EFDs) leo, Jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabishara Bw. Johnson Minja na Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mzee Benard Mchovu. (Picha zote na Regnihaldah Mpete-TRA)
Na Anitha Jonas – MAELEZO.
SERIKALI imefikia muafaka katika mgogoro wake na wafanyabiashara juu ya matumizi ya mashine za kieletroniniki EFD’s.
Hayo ameyasema leo Waziri wa Fedha Mhe.Saada Mkuya alipokuwa akitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari juu ya Serikali kufikia muafaka wa makubaliano yaliyofanyika kwa ushirikiano wa Kamati kuu ya Taifa iliyoshirikisha wajumbe kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na Viongozi wa Jumuiya ya wafanyabiashara katika ngazi ya Taifa.
“Matumizi ya mashine za EFD yalipoanza yalileta changamoto kwa wafanyabiashara ,hivyo niliunda kamati ya kitaifa pamoja na kamati katika ngazi za Mikoa na Wilaya pamoja na wenyeviti wakuu wa mikoa kutafuta suluhu la suala hili”alisema Mhe. Mkuya.
Waziri Mkuya aliendelea kusema Kamati imetoa mapendekezo mbalimbali kwa Serikali ikiwemo ya muda mfupi ambayo wameshaanza kuyafanyia kazi na mengine ni yakisera ambayo yatahitaji muda mrefu yatafuata utaratibu unaopaswa katika utekelezaji wake,kwa ufuatiliaji na ushirikiano wa karibu,kupitia kamati ya Kitaifa itakayodumu kwa kipindi cha miaka miwili.
Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara nchini Bw. Johnson Minja aliipongeza serikali kwa kubali kukaa meza moja na wafanyabiashara katika kutatua mgogoro huo uliyokuwepo katika matumizi ya mashine za EFD na kuakukubali kupokea changamoto za wafanyabiashara na kuahidi kuzifanyia kazi.
“Serikali imekubali kupitia mfumo wa utozwaji kodi kuanzia ngazi ya bandarini na kuongeza uwazi ilikuleta uelewa kwa wafanyabiashara na kuepuka kutozwa kodi kubwa kutoka na kukosa uelewa wa gharama za ulipaji kodi”,alisema Bw.Minja.
Aidha Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo ya wafanyabiashara aliendelea kusema ni wajibu wa kila mmoja kulipa kodi na hii ni kwa maendeleo ya nchi na pia ni kosa kwa mfanyabiashara yoyote kuendesha biashara yake bila kuwa na namba ya utambulisho wa mlipakodi (Tin Number), tunataka namba ya walipakodi iendelee kuongezeka na kuondoa kabisa wafanyabiashara wasio lipa kodi.
Mbali na hayo nae Kamishana Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Rished Bade aliipongeza kamati kwa kuweza kufika mwafaka na kuweza kuzitambua changamoto mbalimbali zilizokuwa zikiwasumbua wafanyabiashara na ameahidi, kuwa ofisi yake itaendelea kuwawajibisha watu wote wanao kiuka taratibu za ulipaji kodi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment