TANGAZO


Thursday, June 4, 2015

Mkuu wa Wilaya Igunga awaambia wananchi “Chonde chonde fichueni wanaoficha wenye maradhi ya Fistula”

Wakazi wa Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora, wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya hiyo, Mh. Zipporah Pangani, alipokuwa akiwaelewesha juu ya maradhi ya Fistula wakati wa kampeni ya kutoa elimu kuhusiana na maradhi hayo wilayani humo. Kampeni hiyo inayoendeshwa na Hospitali ya CCBRT na Vodacom Foundation inaendelea kufanyika katika mikoa mitatu kuwasisitiza wanaume  kuwaruhusu akina mama kujitokeza  ili wakatibiwe maradhi hayo kwani yanatibika. Inakadiriwa ni wastani ya wanawake 3,000 kwa mwaka hupatwa na maradhi hayo wanapojifungua. (Na Mpigapicha wetu)
Mkuu wa Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora Mh.Zipporah Pangani (katikati) akimsikiliza kwa makini  Mwajuma Rashid wakati alipokuwa akiwasomea  moja ya kipeperushi  kuhusiana na ugonjwa wa Fistula. Kampeni hiyo inayoendeshwa na Hospitali ya CCBRT na Vodacom Foundation  inaendelea kufanyika katika mikoa mitatu kuwasisitiza wanaume  kuwaruhusu wakina mama kujitokeza  ili wakatibiwe maradhi hayo kwani yanatibika. Inakadiriwa   wastani ya wanawake 3,000 kwa mwaka hupatwa na maradhi hayo  wanapojifungua. 
Mkuu wa Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora Mh. Zipporah Pangani (katikati) na Meneja Biashara Idara ya Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Grace Lyon (kushoto)wakimsikiliza   Meneja Mawasiliano wa Hospitali ya CCBRT Abdul Kajumulo, wakati wa kampeni ya kutoa elimu kuhusiana na maradhi ya  Fistula yanayowakabili wanawake hapa nchini. Kampeni hiyo inayoendeshwa na Hospitali ya CCBRT na Vodacom Foundation  inaendelea kufanyika katika mikoa mitatu. Inakadiriwa  wastani ya wanawake 3,000 kwa mwaka hupatwa na maradhi hayo  wanapojifungua. 
Baadhi ya wakazi wa Wilaya ya Igunga MKoani Tabora waliojitokeza kwenye uwanja wa Sokoine wakati wa kampeni ya kutoa elimu kuhusiana na maradhi ya  Fistula yanayowakabili wanawake hapa nchini. Kampeni hiyo inayoendeshwa na Hospitali ya CCBRT na Vodacom Foundation  inaendelea kufanyika katika mikoa mitatu nchini kuwataka wanawake wenye maradhi hayo kujitokeza kupata matibabu. Inakadiriwa   wastani ya wanawake 3,000 kwa mwaka hupatwa na maradhi hayo wanapojifungua.
Mmoja wa wasanii wa kundi la Mjomba Bendi, Maria John akiigiza kwa hisia kali  kwa wakazi wa Igunga waliofurika katika  uwanja wa Sokoine wakati wa kampeni ya kutoa elimu kuhusiana na maradhi ya  Fistula yanayowakabili wanawake hapa nchini, Kampeni hiyo inayoendeshwa na Hospitali ya CCBRT na Vodacom Foundation  inaendelea kufanyika katika mikoa mitatu  kuwasisitiza akina  mama wenye maradhi hayo kujitokeza kutibiwa. 
Wanafunzi wa kidato cha tatu shule ya sekondari ya Igunga Mkoani Tabora, Asha Omari (kushoto) na Fatma Juma wakisoma kipeperushi walichogawiwa wakati wa kampeni ya maradhi ya Fistula iliyofanyika mkoani humo. Kampeni hiyo inayoendeshwa na Hospitali ya CCBRT na Vodacom Foundation  inaendelea kufanyika katika mikoa mitatu ya hapa nchini na akina mama wenye maradhi hayo wanahimizwa kujitokeza wakatibiwe. Inakadiriwa   wastani ya wanawake 3,000 kwa mwaka hupatwa na maradhi hayo wanapojifungua.

No comments:

Post a Comment