Ofisa wa Mfuko wa Pensheni PSPF Tawi la Zanzibar Hazina Konde akimkabidhi msaada wa magodoro Mbunge wa Jimbo
la Chumbuni Zanzibar, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe Ame Perera kwa ajili ya Wananchi waliopata maafa ya
mvua na kuharibikiwa na mali zao, makabidhiano hayo yamefanyika katika viwanja
vya skuli ya mabanda ya ngome chumbuni Zanzibar.
Ofisa wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF Tawi la Zanzibar Hazina Konde akitowa maelezo kwa niaba ya
Mkufugenzi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi
msaada wa Magodoro kwa wananchi wa Jimbo la Chumbuni waliopata janga la mvua za
masika katika shehia tatu za jimbo hilo, Chumbuni. Karakana na Muembemakumbi
Zanzibar.
Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe Perera Ame Silima akitowa shukrani kwa
uongozi wa Mfuko wa PSPF kwa msaada wao kwa Wananchi wa Jimbo lake wakati wa
makabidhiano hayo yaliofanyika katika viwanja vya skuli ya mabanda ya ngombe
chumbuni Zanzibar.Mhe Mbunge akiishukuru PSPF kwa kutumia sehemu ya pato lake
kwa kusaidia Jamii.
Sheha wa Shehia ya Karakana Ndg Bakari Makame akitowa shukrani kwa niaba ya
wananchi wake kwa Msaada wa Magodoro yaliotolewa na Mfuko wa PSPF kwa kujali
wananchi wakati wa maafa na kutowa
shukara hizo kwa Uongozi huo wakati wa makabidhiano ya msaada huo yaliofanyika
katika viwanja vya Skuli ya Mabanda ya Ngome Chumbuni Zanzibar.
Wananchi wa Shehia tatu za Jimbo la Chumbuni Zanzibar
wakimsikiliza Ofisa wa Mfuko wa PSPF Tawi la Zanzibar Bi Zahazia Konde akitowa
maelezo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mfuko huo kwa wananchi wa Jimbo la Chumbuni
Zanzibar wakati wa kutoa msaada wa magodoro kwa wananchi waliopata maafa ya
mvua hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment