Mkurugenzi wa Exclusive Media, Godie Gervas, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu maonesho ya asasi za kifedha yatakayoandaliwa na taasisi hiyo kwa kushirikiana na Kampuni ya Qutub Global, yajulikanayo kwa jina la Pesa Expo, yatakayofanyika mwanzoni mwa mwezi wa Septemba, mwaka huu, jijini. Kushoto ni Mtaalamu wa Biashara za Kimataifa wa taasisi hiyo, Raymunda Mhenga na kulia ni Mkurugenzi Mwenza wa taasisi hiyo, Sunday Mashelle.
Mkurugenzi wa Exclusive Media, Godie Gervas, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu maonesho ya asasi za kifedha yatakayoandaliwa na taasisi hiyo kwa kushirikiana na Kampuni ya Qutub Global, yajulikanayo kwa jina la Pesa Expo, yatakayofanyika mwanzoni mwa mwezi wa Septemba, mwaka huu, jijini. Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Qutub Global, Jeremia Fumbe na katikati ni Mtaalamu wa Biashara za Kimataifa wa taasisi hiyo, Raymunda Mhenga.
Mtaalamu wa Biashara za Kimataifa wa taasisi ya Exclusive Media, Raymunda Mhenga (kushoto), akifafanua jambo, kuhusu maonesho hayo, wakati wa mkutano huo. Katikati ni Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Godie Gervas na kulia ni Mkurugenzi Mwenza wa taasisi hiyo, Sunday Mashelle.
Mtaalamu wa Biashara za Kimataifa wa taasisi ya Exclusive Media, Raymunda Mhenga (kushoto), akifafanua jambo, kuhusu maonesho hayo, wakati wa mkutano huo. Katikati ni Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Godie Gervas.
EXCLUSIVE Media
(T) Ltd ikishirikiana na Qutub
Global Ltd imeandaa maonyesho makubwa yaTaasisi na asasi za kifedha nchini
Tanzania yajulikanayo kama Pesa Expo.
Maonyesho hayo yanatarajiwa kufanyika mwanzoni
mwa mwezi wa tisa jijini Dar es salaam.
Pesa Expo itahusisha Taasisi na asasi mbali
mbali za kifedha Kama
1.
Mabenki
2.
Saccos
3.
Makampuni ya bima
4.
Makampuni yanayotoa huduma za Mikopo
(Microfinance)
5.
Makampuni yanotoa huduma za fedha za
kieletroniki
6.
Mifuko ya hifadhi ya jamii
7.
Makumpuni yanoyotoa huduma za kutuma
fedha
8.
Soko la hisa na madalali wake
9.
Makampuni yanayotoa huduma za
ushauri wa kifedha
10. Taasisi
zisizo za Faida zinazotoa Elimu kuhusu mambo ya fedha (NGOs)
Tafiti nyingi zinaonyesha kuwa watanzania wana
ufinyu wa elimu ya kutosha juu ya huduma nyingi za kifedha zitolewazo nchini
pamoja na faida zake.
Lengo kuu la Pesa Expo ni kuwakutanisha watoa
huduma za kifedha pamoja na watumiaji wao na wananchi kwa ujumla.
Pesa Expo inapenda kuchukua nafasi hii kutoa
wito kwa asasi zote za kifedha nchini kushiriki maonyesho hayo.
Tayari baadhi ya makampuni yamesha thibitisha
ushiriki wao hivyo tunaendelea kutoa wito kwa wale ambao bado hawajathibitisha
kuendelea kujitokeza na kuthibitisha ushiriki wao katika maonyesho haya
Pesa Expo itatoa fursa mbali mbali kwa makampuni
shiriki kama vile
Kufanya mauzo ya moja kwa moja
Kutangaza huduma zao mpya
Kutoa elimu ya huduma za kwa wananchi
Kuboresha mahusiano yao na wateja
Kuboresha mahusiano baina ya makampuni shiriki
Kubadilishana mawazo na wajasiriamali na
wananchi
Kufanya tafiti ya bidhaa zao
Kujitangaza nk
Nimalize kwa kusema Pesa Expo ni maonyesho endelevu yatakayokuwa
likifanyika kila mwaka likianzia Dar es salaam na kuzuunguka mikoa mbali mbali
nchini.
Kwa hiyo tunawakaribisha Taasisi na asasi zote
za kifedha na wadau wote wa masuala ya fedha nchini na wananchi kwa ujumla
kuweza kushirikiana nasi kuweza kufanikisha maonyesho haya.
Asanteni sana.
Mob:
+255 779 888 859, +255 673 400 533
E-mail: pesaexpotz@gmail.com
No comments:
Post a Comment