Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) akizungumza na Waziri wa zamani wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Vijana, Mbunge wa Jimbo la Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka alipowasili katika Kijiji cha Kyamkwikwi wilayani Muleba tayari kwa safari ya kwenda kutembelea visiwa vinne wilayani humo jana.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) akilakiwa kwa furaha na Waziri wa zamani wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Vijana, Mbunge wa Jimbo la Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka alipowasili katika Kijiji cha Kyamkwikwi wilayani Muleba tayari kwa safari ya kwenda kutembelea visiwa vinne wilayani humo jana.
Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akishuka kutoka kwenye boti baada ya kuwasili katika Kisiwa cha Iloba, Kata ya Ibumbile Jimbo la Muleba Kaskazini wakati wa ziara yake mkoani Kagera jana.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akishuka kutoka kwenye boti baada ya kuwasili katika Kisiwa cha Iloba, Kata ya Ibumbile Jimbo la Muleba Kaskazini wakati wa ziara yake mkoani Kagera jana.
Komredi Kinana (wa pili kulia) akishiriki kusomba matofali aliposhiriki ujenzi wa jengo la Shule ya Msingi Iloba, katika Kisiwa cha Iloba, Kata ya Ibumbile, Muleba Kaskazini, mkoani Kagera jana.
Komredi Kinana akishuka kwenye boti baada ya kuwasili katika Kijiji cha Kitungulu, Jimbo la Muleba Kusini akitoka kutembelea visiwa vinne wilayani Muleba, mkoani Kagera jana.
Komredi Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Fatuma, Muleba Mjini jana. (Picha zote na Richard Mwaikenda)

No comments:
Post a Comment