Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi (MB), akiwaonyesha waheshimiwa Wabunge taarifa iliyoambatana na Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi yake kwa mwaka wa fedha 2015/16. (Picha zote na Georgina Misam, Maelezo Dodoma)
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendekeo ya Makazi Mh. William Lukuvi (MB), Bungeni Dodoma leo, akisoma Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara yake kwa mwaka wa Fedha 2015/16.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendekeo ya Makazi Mh. William Lukuvi (MB) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Bw. Nehemiah Mchechu, baada ya kuwasilisha Bungeni bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyimba na Maendeleo ya Makazi leo Dodoma.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendekeo ya Makazi Mh. William Lukuvi (MB) akiteta jambo na Watendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Mkuregenzi Mkuu wa Shirika hilo Bwn. Nehemiah Mchechu (kulia) na Meneja wa Shirika hilo Mkoa wa Dodoma, Bwn. Itandula Gambalagi.
Na Georgina Misam, Maelezo Dodoma
07/06/2015
KATIKA kuboresha mahusiano kati ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu na Tume ya Vyuo Vikuu na kuondosha migomo na maandamano ya wanafunzi dhidi ya Bodi, serikali imeweka muwakilishi wa Tume ya Vyuo Vikuu kuwa mjumbe kwenye Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu.
Akijibu swali Bungeni Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Anne Kilango Malecela amesema pia chuo kimeelekezwa kuajiri Afisa atakayeshughulikia masuala ya mikopo na kuwa kiungo kati ya wanafunzi, Chuo na Bodi ya Mikopo.
Mhe. Malecela alikua akijibu swali lililoulizwa ma Mhe. Suzan Lyimo (Viti maalum) aliyetaka kujua matokeo ya tume maalum iliyoundwa kuchunguza utendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu.
Mhe. Malecela amesema kuwa Tume hiyo ilibaini kuwa pamoja na mambo mengine mawasiliano hafifu kati ya Bodi ya Mikopo, Tume ya vyuo vikuu, Taasisi za Elimu ya juu na Wanafunzi ndio yanasababisha migomo na maandamano ya wanafunzi wa Elimu wa Juu.
Amesema utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa na Tume iliyoundwa kuchunguza yamefanikiwa kuondosha migomo na maandamano hayo.
Aidha, Bodi ya Mikopo imeboreshwa kwa kuajairi watumishi wenye sifa stahiki na vitendea kazi vya kutosha. Aidha, Bodi ya Mikopo imeanzisha ofisi katika kanda za Dododma, Zanzibar na Mwanza ili kuwahudumia wadau wa karibu.

No comments:
Post a Comment