Mratibu Maafa, Idara ya uratibu maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Benedict Kisaka akitoa mafunzo ya menejimenti ya maafa wakati wa mafunzo kwa Waratibu maafa mkoani Kagera tarehe 24 Juni, 2015.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Kagera, Fikira Kisimba (katikati), akifuatilia mafunzo ya menejimenti ya maafa wakati wa mafunzo kwa waratibu maafa mkoani Kagera tarehe 24 Juni, 2015, (mwenye miwani) ni Mkurugenzi msaidizi (Mipango na Utafiti), Idara ya Uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Naima Mrisho.Mwakilishi wa Mkuu wa Polisi wilaya ya Bukoba, Mkaguzi John Kayunga akifafanua masuala ya menejimenti ya maafa katika Jeshi la Polisi mkoani Kagera wakati wa mafunzo ya menejimenti ya maafa kwa waratibu maafa mkoani Kagera tarehe 24 Juni, 2015.
Mratibu maafa wilayani Muleba Mkoani Kagera, Ruth Ishabakaki akifafanua masuala ya menejimenti ya maafa wilayani Muleba wakati wa mafunzo ya menejimenti ya maafa kwa waratibu maafa mkoani Kagera tarehe 24 Juni, 2015, mafunzo hayo yameratibiwa na Idara ya Uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu.
Baadhi ya waratibu Maafa mkoani Kagera wakifuatilia mafunzo ya menejimenti ya maafa kwa waratibu hao tarehe 24 Juni, 2015, mafunzo hayo yameratibiwa na Idara ya Uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu.
Na Mwandishi Maalum
KAMATI za kuratibu maafa
katika ngazi ya serikali za mitaa zimetakiwa kutekeleza majukumu yao kikamilifu
ya menejimenti ya maafa ili kuweza kujenga jamii yenye uwezo wa kuzuia na
kukabili maafa yanayotokea katika maeneo yao.
Akifungua mafunzo ya waratibu wa maafa mkoani Kagera, tarehe 24
Juni, 2015, Kaimu Katibu Tawala wa mkoa
huo, Fikira Kisimba alieleza kuwa nguvu ya uwezo wa jamii kuweza kukabili
maafa itapatikana iwapo kamati za kuratibu maafa katika ngazi za serikali za
mitaa zitawajibika wakati wote kwa kutokuwa zinasubiri uratibu wa maafa yanapotokea.
“Tunazo kamati za maafa
kuanzia ngazi za vijiji , vitongoji, kata , wilayani hadi mkoani lakini kamati
hizi zinasikika sana wakati maafa yanapotokea hali ambayo si nzuri katika hatua
za menejimenti ya maafa, kwani tunaposema menejimenti ya maafa tunazingatia,
kuzuia, kukabili maafa na kurejesha hali
ya awali baada ya maafa kutokea” alisema Kisimba.
Kisimba aliongeza kuwa mkoa
wa Kagera umekuwa ukikumbwa na maafa ya upepo mkali ambapo alibainisha kuwa
wilaya ya Muleba imewahi kupatwa na maafa hayo pamoja na maafa ya Kimbunga
katika kisiwa cha Goziba lakini wilayani Misenyi magonjwa ya mlipuko yamekuwa
yakijitokeza hivyo kamati husika zikiwajibika athari za maafa haya zinapunguzika.
Awali akiongea katika
mafunzo hayo, Mkurugenzi msaidizi (Mipango na Utafiti), Idara ya Uratibu maafa Ofisi
ya Waziri Mkuu, Naima Mrisho alizitaka kamati za serikali za
mitaa na vijiji mkoani humo
kuhusisha maafa na mipango yao ya maendeleo, ili kuhakikisha jamii inakuwa na
uwezo wa kupunguza athari za maafa hayo.
“Ili kamati za maafa ziweze
kuwajibika ipasavyo hatunabudi Mipango ya maendeleo katika serikali za mitaa ihusishe
maafa ili jamii iwe na uwezo wa kukabiliana na maafa wakati janga linapotokea
na wakati wa kurejesha hali. Kamati za ” alisisitiza Mrisho.
Ofisi ya
Waziri Mkuu, kupitia Idara ya Uratibu
Maafa itaendelea kutoa elimu na kushirikisha Wadau ili
kuimarisha uwezo wa nchi katika kujenga uwezo wa kuzuia, kupunguza na
kukabiliana na athari za maafa yanapotokea.

No comments:
Post a Comment