Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Bw. Felix Ngamlagosi (kushoto) akionesha tuzo ya mdhibiti bora wa mwaka wa nishati iliyotolewa kwa mamlaka hiyo na Jukwaa la Nishati Afrika wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Umeme kutoka mamlaka hiyo, Anastas Mbawalla.
Mkurugenzi wa Umeme kutoka mamlaka hiyo, Anastas Mbawalla (kulia), akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Bw. Felix Ngamlagosi. (Picha na Salma Ngwilizi –Maelezo)
Na Magreth Kinabo- maelezo
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imebuka mshindi wa mashindano ya Tuzo ya Mdhibiti Bora wa mwaka wa Nishati ya 2015.
Hayo yalisemwa leo na Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Bw. Felix Ngamlagosi wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu tuzo hiyo iliyotolewa na Jukwaa la Nishati la Afrika.
Tuzo hiyo ambayo ilitolewa Juni 8, mwaka huu kwenye sherehe ya mkutano mkuu wa kila mwaka uliofanyika Juni 8 hadi 11 mwaka huu Dubai,Umoja wa Falme za Kiarabu.
“Jopo la wataalamu la wanaofanya kazi kwa kushirikiana na shirika la EnergyNet la Uingereza lilikaa na kuchagua EWURA kuwa ndio mshindi wa kwanza wa mwaka 2015 katika kundi la wadhibiti,’’ alisema Ngamlagosi.
Ngamlagosi alisema tuzo hiyo ni ya mara ya kwanza kutolewa nchini imepatikana baada jopo hilo kuangalia vigezo vya kufanya kazi vizuri, kutoa maelekezo kwa wadau kwa ufasaha bila mabadiliko, na kueleweka kwa wadau. Pia mamlaka hiyo imeandaa kanuni mbalimbali ambazo ni za uzalishaji na uuzaji umeme, usafirishaji umeme na kusambaza umeme zikiwemo leseni.
Aliongeza kwamba tuzo hiyo inafanya Tanzania kutambulika kimataifa kama ni nchi yenye taasisi thabiti ya uhakika ya udhibiti wa sekta ya nishati na maji ambalo ni jambo muhimu kwa nchi kuendelea kuimarisha wawe
Alisema Tanzania sasa itashuhudia upatikanaji wa kiwango cha juu cha mitaji ya uwekezaji kutoka nje ya nchi (FDIs)kwenye sekta za nishati na maji ,ambazo zitavutia uwekezaji zaidi kwenye sekta zingine kwa kuzingatia kutegemeana kwa sekta kati ya sekta ya nishati zingine kiuchumi.
Hivyo Tanzania ipata wawekezaji wa umeme mijini na vijijini kutokana na kuwepo kwa mfumo imara na uwazi unaoleweka katika sekta hiyo.
Ngamlagosi alizitaja taasisi zingine zilizoshirikia kwenye shindano hilo ni Mamlaka ya Udhibiti wa Umeme Cameroon(AESEL) Kamisheni ya Udhibiti wa Umeme na Maji ya Mali (CREE) Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati ya Uganda(ERA)na Kamisheni ya Udhibiti wa Nishati ya Kenya(ERC).
Aliongeza kuwa Tanzania ilishiriki kuandika kitabu cha mikataba ya kuuziana umeme, ambapo Mkurugenzi wa Umeme , Anastas Mbawalla alishiriki pamoja na japo la wataalamu, ambacho kinatarajiwa kuzinduliwa mwishoni mwa mwezi Julai mwaka huu.

No comments:
Post a Comment