Mkurugenzi wa wa EACOM Africa, David Silomba (kulia) akikabidhi hundi ya thamani ya sh. milioni 10 kwa Mwenyekiti wa Kituo cha New Hope Family Group Omari Kombe (kushoto) na katikati ni Kampeni Meneja, Braiton Balige.
Na Salma Ngwilizi- Maelezo
KITUO cha kulelea watoto waishio mazingira magumu New Hope Family Group kilichopo kisarawe II-kigamboni, kimewaomba wagombea urais nchini, kuzungumzia suala la kusaidia watoto yatima katika ahadi zao.
Kauli hiyo imetolewa leo na Meneja wa kampeni hiyo Bw.Braiton Balige wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu ujenzi wa kituo ambacho kinasaidia jumla ya watoto 154 .
“Tumezoea kuwa jukumu la watoto waishio katika mazingira magumu ni la Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Wizara ya Maendeleo ya Jamii, jinsia na Watoto, NGO’s, Taasisi za kidini na watu binafsi pekee,lakini kuna kundi muhimu sana halijahusishwa kundi hilo kama lingehusishwa tungeweza kutatua kabisa matatizo ya watoto waishio katika mazingira magumu,kundi hili ni la wanasiasa.’’alisema Braiton.
Aliongeza kuwa wameanzisha kapu maalum kwa watangaza nia katika nafasi ya urais kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho, ambacho kitasaidia kukuza vipaji vyao na kisha kuwawezesha kunza miasha.
Katika kusindikiza kampeni hiyo Bw. David Silomba Mkurugenzi BEACOM AFRICA alichangia kwa kutoa hundi yenye thamani ya kiasi cha shilingi milioni 10.
Katika kufanikisha kukusanya michango hiyo kamati maalumu itakuwepo viwanja vya leaders club kinondoni Juni 20 na 21mwaka huu kwa ajili ya kupokea michango kutoka kwa wadau mbalimbali wanaowaunga mkono wagombea.

No comments:
Post a Comment