England imefanya uamuzi sahihi kuwaondoa katika michuano ya ubingwa wa Ulaya kwa wachezaji wa umri chini ya miaka 21, baadhi ya wachezaji wake ambao wanacheza ligi kuu ya nchi hiyo, amesema mkurugenzi wa chama cha soka wa maendeleo ya wachezaji Dan Ashworth.
Timu ya England chini ya kocha Gareth Southgate ilifuzu kucheza hatua ya makundi kwa kwenda Jamhuri ya Czech.
"Tulifanya uamuzi na nautetea ," Ashworth amemwambia mwandishi mwandamizi wa BBC wa habari za mpira wa miguu Ian Dennis.
"Timu za vijana zipo kusaidia kuwakuza wachezaji na kuwapa uzoefu kuingia katika timu ya wakubwa."
Mchezaji wa ushambuliaji wa Liverpool Raheem Sterling, kiungo wa Everton Ross Barkley, viungo wa Arsenal Alex Oxlade-Chamberlain na Jack Wilshere na mlinzi wa Manchester United Phil Jones ni miongoni mwa wachezaji waliokuwa wakihitajika katika timu hiyo, lakini hawakuitwa.
England, ambayo ilikuwa na wachezaji wa ligi kuu, akiwemo mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane, mlinzi wa Everton John Stones na mshambuliaji mpya wa Liverpool Danny Ings, ilipoteza kwa Ureno 1-0 , wakaifunga Sweden kwa idadi kama hiyo lakini ilipoteza 3-1 kwa Italia.
No comments:
Post a Comment