TANGAZO


Sunday, May 10, 2015

Waandamanaji wapuuza agizo Burundi

Rais wa Burundi PIerre Nkurunziza akiwasilisha stakhabadhi zake za kutaka kuwania urais kwa muhula wa tatu
Wapinzani wa raisi wa Burundi Pierre Nkurunziza wamepuuza agizo la serikali la kuwataka wasitishe maandamano ya wiki mbili wakilitaja agizo hilo kuwa sawa na kutangaza vita.
Hadi sasa watu 18 wameuawa tangu rais Nkurunziza atangaze kuwa atawania muhula wa tatu kwenye uchaguzi wa mwezi ujao.
Waandamanaji wachoma matairi katika vizuizi vya barabarani kupinga hatua ya Nkurunziza ya kuwania muhula wa tatu
Katika maeneo mengine waandamanaji waliweka vizuizi katika barabara usiku kucha kinyume na agizo la serikali ambalo lilitolewa siku ya jumamosi kwamba vizuizi vyote viondolewe katika kipindi cha saa 48.
Habari zinazotufikia zinasema kuwa watu wawili zaidi wamedaiwa kuuawa katika maandamano hayo na kuongeza idadi ya waliouwa kufikia 20.

No comments:

Post a Comment