Ubelgiji imesitisha msaada wa aina yoyote kwa Burundi, hasa uliokuwa ukifadhili uchaguzi mkuu wa nchi hiyo.
Hayo ni kutokana na mapigano makali ambayo yanashuhudiwa kwa sasa nchini humo, kati ya polisi na raia wanaopinga hatua ya rais Pierre Nkurunziza ya kuwania tena urais kwa muhula wa tatu.
Ghasia zimekuwa zikitokea nchini humo tangu rais alipotangaza hatua hiyo ya kuwania tena kiti hicho kinyume na katiba ya nchi hiyo.
Mchunguzi mmoja wa jumuia ya bara Ulaya, alisema juma lililopita kuwa, masharti ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu yameafikiwa.
Bwana Nkurunziza anazindua kampeini yake ya kuwania kiti hicho hii leo Jumatatu.
Umoja wa mataifa umeelezea kuongezeka kwa idadi ya watu wanaoitoroka Burundi.
Kufikia sasa zaidi ya watu elfu mia moja na hamsini wamekimbia nchi hiyo huku zaidi ya watu 19 wakiuwawa katika ghasia.
No comments:
Post a Comment