TANGAZO


Monday, May 11, 2015

Rais wa Somaliland aongezewa muda

Rais wa jamhuri ya Somaliland Ahmed Silanyo
Kumekuwa na maandamano katika jamhuri iliojitangaza ya Somaliland baada ya mda wa kuongoza wa raia Ahmed Silanyo kuongezwa kwa miaka miwili.
Baraza la wazee lilipiga kura ya kuahirishwa kufanyika kwa uchaguzi uliotarajiwa kufanyika mwezi ujao likisema kuwa usajili wa wapigaji kura hautakamilika kwa wakati unaofaa.
Muda wa bunge pia uliongezwa.
Somaliland ilitangaza kupata uhuru kutoka kwa Somalia miaka 24 iliopita lakini ilikuwa haijatambulika kimataifa.

No comments:

Post a Comment