TANGAZO


Sunday, May 10, 2015

Rais Dk. Shein awajulia hali majeruhi, ahudhuria mazishi ya Wana-CCM waliofariki kwa ajali ya gari Kisiwani Unguja

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein akishiriki katika swala ya maiti kumswalia Bi. Mwanaidi Zamir Haji miaka 28 mkaazi wa Magogoni Mjini Unguja leo. Marehemu alifariki kwa ajali ya  gari iliyopinduka huko  Mtowapwani Kaskazini jana. (Picha zote na Ikulu)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein akitia udongo katika kaburi la Marehemu Bi. Mwanaidi Zamir Haji miaka 28 mkaazi wa Magogoni Mjini Unguja aliyefariki kwa ajali ya gari iliyopinduka huko  Mtowapwani Kaskazini jana na kuzikwa leo katika makaburi ya Mwanakwerekwe.
Baadhi ya wananchi na waumini wa Dini ya Kiislamu walioshiriki katika maziko wakimuombea Marehemu Bi. Mwanaidi Zamir Haji miaka 28 mkaazi wa Magogoni Mjini Unguja aliyefariki kwa ajali ya gari iliyopinduka huko Mtowapwani Kaskazini jana na kuzikwa leo katika makaburi ya Mwanakwerekwe.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na ndugu wa Marehemu Bi. Mwanaidi Zamir Haji miaka 28 mkaazi wa Magogoni Mjini Unguja  baada ya mazishi yaliyofanyika leo makaburi ya Mwanakwerekwe. Marehemu alifariki kwa ajali ya gari iliyopinduka jana huko  Mtowapwani Kaskazini A Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein akimfariji Salhia Sheha Khamis, mkaazi wa Kwamtipura aliyelazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja jana baada ya kupata ajali ya kupinduka kwa gari iliyobeba wana-CCM wakitokea Nungwi katika shuhuli za kichama. Katika ajali hiyo watu watatu wamefariki Dunia.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein akimfariji Bi. Mauwa Ali  Khamis, mkaazi wa Kwamtipura aliyelazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja jana baada ya kupata mshtuko wa ajali ya kupinduka kwa gari iliyobeba wana-CCM wakitokea Nungwi katika shughuli za kichama ambapo watu watatu wamefariki Dunia katika ajali hiyo.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai alipokuwa akitoa maelekezo kwa watendaji wa Chama katika Hospitali ya Mnazi Mmoja jana, alipoungana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein kuwafariji Wanachama wa CCM waliolazwa baada ya kupata ajali ya kupinduka kwa gari walilopanda wakitokea Nungwi katika shughuli za kichama. Katika ajali hiyo, watu watatu wamefariki Dunia.
Baadhi ya Wananchi na wana-CCM wakibeba jeneza la Marehemu Bi. Munira Abdalla, mkaazi wa Mkele, Mjini Unguja aliyefariki kwa ajali iliyotokea jana Mkokotoni, Mtowapwani kwa kupinduka na gari walilokuwa wamepanda wakitokea Nungwi. Marehemu amezikwa leo, makaburi ya Mwanakwerekwe Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein na Waziri Kiongozi Mstaafu Shamsi Vuai Nahodha waliongana na wananchi na wana-CCM katika maziko ya marehemu Bi. Munira Abdalla, mkaazi wa Mkele aliyefariki kwa ajali iliyotokea jana Mkokotoni, Mtowapwani kwa kupinduka na gari waliokuwa wamepanda wakitokea Nungwi. Marehemu amezikwa leo makaburi ya Mwanakwerekwe Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein na Waziri Kiongozi mstaafu, Shamsi Vuai Nahodha, wakiwa na waombolezaji katika kumuombea dua marehemu Bi. Munira Abdalla, mkaazi wa Mkele aliyefariki kwa ajali iliyotokea jana Mkokotoni, Mtowapwani kwa kupinduka na gari walilokuwa wamepanda wakitokea Nungwi. Marehemu amezikwa leo katika makaburi ya Mwanakwerekwe Mjini Unguja

Na Said Ameir, Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amehudhuria mazishi ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi-CCM Wilaya ya Mjini waliofariki kwa ajali ya gari iliyotokea jana huko Mkototoni, Wilaya ya Kaskazini ‘A’ Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Wanachama hao walikuwa wakitokea kijiji cha Nungwi ambako walikwenda kufanya mafunzo kwa vitendo ikiwa ni sehemu ya Mafunzo ya Darasa la Itikadi ambayo wamekuwa wakihudhuria.

Katika ajali hiyo iliyotokea katika kijiji cha Mto wa Pwani Mkokotoni watu watatu walifariki dunia na wengine kujeruhiwa ambapo wawili kati yao bado wamelazwa katika hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja mjini Unguja.

Dk. Shein alishiriki mazishi ya Bi Mwanaidi Zamir Haji na Bi Munira Abdalla wote wakaazi wa Mkele Wilaya ya Mjini. Mazishi yao yaliyofanyika kwenye makaburi ya Mwanakwerekwe kwa nyakati tofauti.

Mwana CCM mwingine aliyefariki ni Bibi Mwanahawa Haji Machano mkaazi wa Shaurimoyo mjini Unguja na mazishi yake yamefanyika kijijini kwao Mkwajuni.

Dk. Shein ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar aliwatembelea na kuwafariji majeruhi waliolazwa katika hospitali ya Mnazi Mmoja kutokana na ajali hiyo pamoja na wagonjwa wengine waliolaza katika wodi za akimamama walikolazwa majeruhi hao.   
Majeruhi hao ni Bi Salhia Sheha Khamis wa Kwamtipura, Bi Sawade Haji Khamis mkaazi wa Shaurimoyo na Bi Mauwa Haji Khamis ambaye amelazwa kutokana na mshituko alioupata baada ya  taarifa za ajali hiyo.

Mazishi hayo yalihudhuria na viongozi na mamnia ya wananchi akiwemo Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali vuai.

No comments:

Post a Comment