Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi wa Sita kutoka kushoto akijumuika pamoja na waumini wa dini ya Kiislamu katika kumsalia Marehemu Mwanahawa Ali Machano aliyekuwa Mwenyekiti wa UWT Tawi la Shauri Moyo Mjini Zanzibar. Kulia ya Balozi Seif ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kaskazini Unguja Nd. Haji Juma Haji Marehemu Mwanahawa aliyezikwa kijijini kwao Uyagu Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja alikuwa miongoni mwa wanafunzi watatu wa darasa la Itikadi la CCM waliokuwa wakitokea Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja kwa zira za Kimasomo. (Picha na Hassan Issa – OMPR – ZNZ)
Na Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
10/5/2015.
MJUMBE wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi Balozi Seif Ali Iddi leo alijumuika pamoja na wana CCM, Wananchi pamoja na Wana Familia katika Mazishi ya Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Tawi la Shauri Moyo Bibi Mwanahawa Ali Machano.
Maziko ya Bibi Mwanahawa Ali aliyefariki Dunia jana jioni kufuatia ajali ya Gari iliyotokea Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja yamefanyika kijiji kwao Uyagu Mkwajuni Wilaya ya Kaskazini “ A “.
Mwenyekiti huyo wa UWT Tawi la Shauri Moyo alikuwa miongoni mwa wanafunzi watau wa Darasa la Itikadi la Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Amani waliofariki Dunia wakitokea katika ziara ya kimasomo Nungwi Mkoani humo.
Baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo walieleza kwamba Basi lililokuwa likiwasafirisha wanafunzi hao wa Darasa la Itikadi lilipatwa na mtihani huo wakati Dereva wa Gari hiyo alipojaribu kulikwepa Gari la Ng’ombe lililokatisha bara bara ghafla katika maeneo ya karibu na chuo cha Amali Mkokotoni.
Marehemu Mwanahawa Ali Machano ameacha Mume na watoto sita. Mwenyezi Muungu alilaze roho ya marehemu mahali pepa peponi. Amin.
No comments:
Post a Comment