Kocha wa klabu ya Real Madrid, Carlo Ancelotti amekataa kuzungumzia mustakabali wake kufuatia kikosi chake kutolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya jana.
Madrid ilishindwa kupindua matokeo ya kufungwa mabao 2-1 katika mchezo wa mkondo wa kwanza dhidi ya Juventus baada ya kujikuta wakipata sare ya bao 1-1 na kuwafanya mabingwa hao wa Serie A kusonga mbele kwa jumla ya mabao 3-2.
Akihojiwa mara baada ya mchezo huo, Ancelotti amesema ni mapema mno kuzungumzia mustakabali wake kwani bado msimu haujamalizika.
Juventus inatarajia kupambana na Barcelona katika mchezo wa fainali utakaofanyika Juni 6 mwaka huu katika Uwanja wa Olimpiki jijini Berlin, Ujerumani.
Mara ya mwisho Juventus kutinga fainali ya michuano hiyo ilikuwa mwaka 2003 wakati walipofungwa na AC Milan.
No comments:
Post a Comment