Waziri wa maswala ya ndani nchini Nepal anasema kuwa idadi ya watu waliofariki katika tetemeko la ardhi Nchini humo, imepanda na kufikia 96.
Zaidi ya watu elfu mbili mia tano wamejeruhiwa.
Wengi wa waathiriwa walikuwa wenyeji wa Dolakha, mji ulioko karibu na kulikochipukia tetemeko hilo la Jumanne.
Mamia ya wanajeshi wa India na helikopta nne za Marekani wanasaka ndege moja ya kijeshi ya Marekani iliyotoweka wakati wa operesheni ya kusambaza misaada mwezi uliopita.
No comments:
Post a Comment