Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Luteni Msitaafu Chuku Gallawa akizungumza jambo kwenye ufunguzi wa mafunzo ya matumizi ya Mashine za kuandikishia wapiga kura kwa njia ya kielektroniki [BVR] kwenye daftari la kudumu leo.
Mchambuzi Mwandamizi wa Compyuta wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa, Frank Mhando akimuonyesha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Chiku Gallawa moja ya mashine ya BVR kuandikishia wapigakura. (Picha zote na John Banda)
Na John Banda, Dodoma
MCHAMBUZI wa Compyuter Mwandamizi wa Tume ya uchaguzi ya Taifa Frank Mhando amesema changamoto zilizojitokeza katika zoezi la uandikisaji katika Mikoa iliyotangulia ukiwemo Mkoa wa Njombe halitajitokeza katika mkoa wa Dodoma.
Mchambuzi huyo aliyasema hayo alipokuwa akimjibu Mkuu wa Mkoa wa Dodoma aliyetaka kujua iwapo changamoto zilizojitokeza katika zoezi hilo, lililofanyika Mkoa wa Njombe ambapo mashine za BVR zilishindwa kutambua baadhi ya vidole vya wakulima, mara baada ya kufungua mafunzo ya siku 2 ya Uboreshaji wa Daftari la wapiga kura kwa watendaji wa Halmashauri za Wilaya.
Mchambuzi huyo alisema hivi sasa tume ya taifa imeondoa changamoto zote ambazo zilijitokeza katika maeneo ambayo walianza kuandikisha wananchi kwa kutumia mfumo huo wa Kiteknolojia [BVR] baada ya wao kujua nini kilichokuwa kimepungua kwenye mashine hizo.
Mhando alisema Mfunzo hayo ya kuwajengea uwezo linawahusisha maafsa watatu wa kila wilaya ambayo jumla yao ni 27 kwa wilaya zote 7 za mkoa wa Dodoma na yatafanyika kwa siku mbili, ambapo kutoka hapo nao wataenda kuwafunza wasimamizi wa kata ambapo itashuka mpaka kwa waandikishaji wasaidizi.
“Ni kweli zoezi la uandikishaji kwa mujibu wa ratiba ni may 15 mwaka huu lakini inaweza kuongezeka kidogo kutokana na maeneo hayo yote matatu kupata mafunzo kwa siku mbili mbili hivyo pamoja na siku za kusafiri kwenda wilayani itaongezeka siku moja na baada ya hapo zoezi la uandikishaji litaanza.
“Kuhusu mashine hizi kukataa baadhi ya Vidole ni kweli ilikataa kutokana na aina ya kazi ambazo mtu anafanya maana alama hizi za vidole zinamtindo wa kufutika hasa kwa kazi ngumu za vijijini tofauti na za mijini lakini kwa Dodoma na mikoa inayoendelea halitajitokeza kutokana na kugundua cha kufanya baada ya changamoto hiyo kujitokeza”, alisema Mhando.
Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Luten Mstaafu Chiku Gallawa amewataka wasimamizi hao kuwa wazalendo kwani zoezi hilo ni la faida ya nchi.
“Mnatakiwa kushirikiana katika utendaji wa kazi hiyo ya uandikishaji wananchi badala ya kutumia muda mwingi kubishana kama mtu yoyote hajui ni bora kuuliza kuliko kupoteza muda maana kwa sasa kupoteza nusu saa na hasara kubwa kwa sababu hairudi wakati kuna mambo mengi ya kufanya”, alisema
Aidha Gallawa alisema baada ya zoezi hilo kukamilika na baadae kuingia katiaka zoezi la uchaguzi ni vizuri mawakala wa vyama vya siasa kutowaingilia wasimamizi badala yake wao waangalie kama sheria na kanuni zilizowekwa na tume ya uchaguzi zinafuatwa na si vinginevyo.
Amewataka Mawakala wa Vyama vya siasa kutowaingilia wasimamizi katika utendaji wao wa kazi bali wawepo kwa ajili ya kuangalia sheria na kanuni zilizowekwa na tume ya taifa ya uchaguzi ili kufanya zoezi hilo kuwa la uwazi.
No comments:
Post a Comment