Mwadili wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kitivo cha Shule ya Elimu ya Biashara, Dkt. Ulingeta Mbamba (kushoto) na Katibu Mtendaji wa Mfuko wa Kuendeleza zao la Korosho Nchini, Bw. Suleiman Lenga wakionyesha mkataba wa ujenzi wa viwanda vitatu vya korosho katika Wilaya za Mtwara, Tunduru na Mkuranga. Hafla hiyo ilifanyika leo Jumatano (Mei 6, 2015) Jijini Dar es Salaam.
1. Makamu
Mkuu wa Chuo cha Ardhi cha Jijini Dar es Salaam, Prof. Gabriel Kassenga (kulia)
na Katibu Mtendaji wa Mfuko wa Kuendeleza zao la Korosho Nchini, Bw. Suleiman
Lenga wakionyesha mkataba wa ujenzi wa viwanda vitatu vya korosho katika Wilaya
za Mtwara, Tunduru na Mkuranga. Hafla hiyo ilifanyika leo Jumatano (Mei 6,
2015) Jijini Dar es Salaam.
Na Ismail Ngayonga, Maelezo
Dar es Salaam
06. Mei, 2015
MFUKO
wa kuendeleza zao la Korosho nchini umetenga kiasi cha Tsh Bilioni 6 kwa ajili
ya ujenzi wa viwanda vitatu vya kubangulia korosho vitakavyojengwa katika
Wilaya za Mtwara, Tunduru na Mkuranga.
Taasisi
zitakazojenga viwanda hivyo ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kupitia Kitivo cha Biashara na Chuo Kikuu
cha Ardhi (ARU).
Akizungumza
katika hafla ya utiaji saini wa mikataba baina ya mfuko huo na wataalamu
washauri, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko huo, Athuman Nkinde katika bajeti
iliyopo kiwanda kimetengewa kiasi cha Tsh Bilioni 2 na pia fedha hizo
zinatarajia kuongezeka kila mwaka kulingana na mahitaji yatakavyojitokeza.
Nkinde
alisema ujenzi wa viwanda hivyo unatarajia kuanza katika kipindi cha miezi mitatu ijayo ambapo pindi vitakapomalika kila
kiwanda kinataraji kuzalisha tani 10000 kwa mwaka, na kuongeza kuwa Ofisi yake
ina imani kubwa ujenzi wa viwanda hivyo utasaidia kuleta mageuzi makubwa ya zao
la koroho nchini.
Aliongeza
kuwa madhumuni ya kuanzisha viwanda hivyo ni kuliongezea thamani kwa zao la korosho ili liweze kuchangia kikamilifu katika kukuza
uchumi wa nchi pamoja na wakulima wa zao hilo nchini.
Kwa
mujibu wa Nkinde alisema taasisi zilizopewa kazi ya ujenzi wa viwanda hivyo havina budi kutambua ukubwa wa kazi kwani zipo
taasisi nyingi zabuni wa ujenzi huo, hivyo ni wajibu wao kuhakikisha kuwa
Tanzania inanufaika kupitia mradi huo.
“Tumeingia
katika historia mpya leo hii, dunia nzima itasikia taarifa hizi za ujenzi wa
viwanda hivi, hivyo ni wajibu wenu kufanya kazi kwa kuzingatia uwezo wa
kitaaluma mliokuwa nao” alisema Nkinde.
“Tanzania
imekuwa ikisafirisha nje ya nchi korosho ghafi, kwa kujenga viwanda hivi
kutatusaidia kupunguza gharama hizo sambamba na kuongeza thamani ya zao hilo”
Kwa
upande wake Katibu Mtendaji wa Mfuko huo, Suleiman Lenga aliwataka
wataalamuwashauri hao kuzingatia viwango, ubora na muda katika kutekeleza
ujenzi wa miradi hiyo kwani taasisi hizo
zina uzoefu mkubwa katika kusimamia na kundeleza miradi mbalimbali ya maendeleo
nchini.
Alisema
katika mikataba iliyosainiwa, Chuo cha Ardhi
kitahusika zaidi katika kuandaa michoro, ramani na usanifu wa majengo
wakati, Chuo cha Biashara kitahusika katika kuandaa andiko la mradi
litakalohusiana na masuala mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa masoko.
Naye
Mwadili wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika Kitivo cha Elimu ya
Biashara, Dkt. Ulingeta Mbamba alisema taasisi itafanya kazi kwa weledi mkubwa
ili kuhakikisha kuwa ujenzi huo utafikia katika ubora na viwango
vilivyokusudiwa.
“Zao
la korosho limekuwa kwa sasa limekuwa ni zao muhimu kwa uchumi wa Tanzania na
wananchi kwa ujumla, hivyo tutahakikisha kuwa kupitias ujenzi huu zao hili
linazidi kuopngezewa thamani yake” alisema Dkt. Mbamba.
Aidha
Makamu Mkuu wa Taaluma katika Chuo Kikuu cha Ardhi, Prof. Gabriel Kassenga alisema wa Chuo kitahakikisha kuwa viwanda
hivyo vitaleta tija iliyokuwa kwa kukuza uchumi wa Taifa na wakulima wa zao la
koerosho nchini.
No comments:
Post a Comment